HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 11 September 2018

GESI ASILIA MHIMILI UKUAJI WA VIWANDA

Mkurugenzi Mtendaji kutoka Kiwanda cha Knauf ambacho ni kimoja wapo kati ya vinne viliyoingia makubaliano ya matumizi ya gesi asilia baada ya kukamilika ujenzi wa toleo na bomba akipata maelezo utekelezaji wa ujenzi.
---
Mahali popote duniani palipo na gesi asilia pamekuwepo na mageuzi makubwa ya ukuaji wa sekta ya viwanda na kukuza uchumi.lia ipo

Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Jipsam cha Knauf Ndugu Georgios Zachopoulos aliyasema hayo wakati alipoungana katika ziara fuoi iliyofanywa na TPDC na Kampuni yake Tanzu ya Gesi (GASCO) kukagua maendelo ya ujenzi wa toleo jipya la gesi asilia katika Kijiji cha Mwanambaya kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani.

Akiwa mmoja wa watendaji wakuu wa viwanda vinne ambavyo vimekamilisha taratibu zote za kuunganishwa na gesi asilia Ndugu Georgios amekiri kufurahishwa na kazi ambayo TPDC inaifanya ya kuhakikisha kuwa viwanda vilivyopo katika eneo la Mkuranga vinapata gesi asilia.

“Sisi kama Knauf tumefurahishwa sana na kazi zinazofanywa na TPDC hususan hii ya kutujengea toleo la gesi asilia hapa Mwanambaya ili kutuwezesha ku pata gesi asilia ambayo itawezesha kuimarisha shughuli zetu kuwa kiwanda bora chenye kuzalisha bidhaa bora na kwa ufanisi mkubwa”

“Gesi asilia ni bora na safi kwa namna nyingi tu na hivyo inapelekea ufanisi mkubwa wa mashine za viwandani katika uzalishaji au uchakataji mbalimbali na ndio maana mahali ambapo gesi asilia ilipo na inatumika kumekuwepo na ukuaji wa kasi wa viwanda kwa mfano kutokana na gesi asilia hii tunajenga kiwanda kikubwa zaidi Kusini mwa Jangwa la Sahara ambacho kwakuwa uwekezaji wake unalenga kutumia gesi asilia basi Knauf itaokoa kiasi cha dola za kimarekani milioni tatu.”

Akijibu swali la kuhusu kiasi ambacho kiwanda kitaokoa kutokana na matumizi ya gesi asilia Bwana Gergios amesema “kuwa kwenye matumizi ya gesi asilia jambo la msingi zaidi si nini unaokoa katika pesa pekee bali ni kwa kiasi gani kiwanda kinakuwa na ufanisi bora zaidi kiutendaji na kukidhi ubora wa bidhaa na hichi ndicho tunachohitaji kwanza na ni wazi kuwa kuanza kwa matumizi ya gesi asilia katika eneo hili kutakuza kwa kasi sekta ya viwanda na uchumi na haswa tukizingatia kuwa eneo hili limetengwa maalum kwa ajili ya viwanda”.

Wakandarasi wa Kampuni ya CPE wakiendelea na kazi ya kuchomelea bomba la gesi katika eneo ambalo litajengwa na kuungwa toleo la gesi asilia kwa ajili ya kusambaza viwandani.
---
Awali akielezea ujenzi wa toleo hilo la kuunganisha gesi asilia kwenye viwanda vilivyopo Mkuranga, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mha. Kapuulya Musomba ameeleza kuwa kazi hiyo ambayo inahusisha utoboaji wa bomba kubwa la gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam imetokana na tathmini ya gharama za matumizi ya matoleo yaliyopo.

“Maamuzi ya kutoboa bomba hili tumeyafikia baada ya kufanya tathmini ya gharama kati ya kutumia matoleo ambayo yapo kwa sasa na kutoboa hapa ndipo tulipogundua kuwa kutumia matoleo yaliyopo yangetugharimu zaidi ya bilioni 10 kutokana na umbali mrefu yalipo matoleo hayo kiasi ambacho ni kikubwa ikilinganishwa na gharama za kutoboa bomba kuweka toleo na kujenga bomba kupelekea kwa wateja wetu, kazi ambayo gharama yake itakua pungufu zaidi hadi kufikia shilingi bilioni moja za kitanzania.”

Aidha akielezea umuhimu wa mradi huo Mha. Kapuulya Musomba alisema “TPDC itahakikisha utekelezaji wa Uchumi wa Viwanda au Tanzania ya Viwanda unakua halisi na kasi inayoridhisha na ndio maana tumeamua kutoboa bomba hapa na kujenga toleo na bomba la kupeleka gesi asilia kwenye viwanda vilivyopo hapa Mkuranga na kwa sasa viwanda ambavyo vipo tayari tumeshaingia navyo mkataba ni vinne lakini tunalenga kuhudumiua viwanda vingi zaidi vilivyopo sasa na vitakavyokuja baadae”.

Mha. Musomba aliongeza kuwa utoboaji wa bomba hilo katika kijiji cha Mwanambaya unadhihirisha usemi wa uwekezaji wa viwanda unawezekana eneo lolote katika kilomita 551 za bomba la gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam kwa kuwa mbali ya uwepo wa matoleo yapatayo 15 ya gesi asilia yaliyojengwa kwenye bomba hilo, ipo teknolojia ya utoboaji wa bomba sehemu yeyote pale patakapoonekana matumizi ya matoleo yaliyopo yapo mbali zaidi na hivyo kusababisha matumizi ya pesa nyingi kujenga miundombinu kutoka kwenye toleo hadi kwa mteja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad