HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 26 September 2018

DKT ABBASI AKUNWA NA UTENDAJI, MAGEUZI YA RC GEITA

Na Mwandishi Wetu
Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel kwa utendaji wake wa ubunifu na unaolenga kuboresha maisha ya Watanzania.
Dkt. Abbasi ameyasema hayo Jumatano Septemba 25, 2018 akiambata na viongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikali (TAGCO) alipofika Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa huyo katika ziara ya kufuatilia utendaji wa sekta ya habari.
Katika mazungumzo hayo Dkt. Abbasi amemueleza Mhandisi Gabriel kuwa mafanikio hayo ya Geita na mengine ambayo Serikali kwa ujumla inayatekeleza umuhimu yanapaswa kutangazwa na kutetewa kwa kuwa yana manufaa nakubwa kwa wananchi.
Katika mazungumzo RC Gabriel alisema mkoa wake umehakikisha mapato kutoka kwa makampuni ya madini yanatumika kuondoa adha za wananchi katika sekta muhimu kama afya, elimu na wajasiriamali.
Alisisitiza kuwa katika sekta ya Afya wamepanga kuwa kufikia Mei, 2019 zahanati zote mkoani Geita zitakuwa zimekamilika.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikali (TAGCO), Bw. Pascal Shelutete amemuhakikishia Mhandisi Gabriel ushirikiano wa kutosha katika eneo la mawasiliano lengo ni kuhakikisha taarifa za Serikali zinawafikia wananchi.
Aidha, Bw. Shelutete pia amempongeza RC huyo kwa utendaji wake makini na wa kimageuzi  unaowagusa na kuwafunza wengi nchini.
 Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiongea na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel ambapo alimueleza umuhimu wa kutangaza na Kuitetea mafanikio ya Serikali kutokana na manuaa yake kwa wananchi, Mkoani Geita.

 Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akimueleza Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi na Viongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) namna walivyojipanga kuendelea kuhakikisha namna mapato ya madini kutoka katika makampuni yanatumika kuondoa adha za wananchi katika sekta muhimu za Afya, Elimu na Wjasiriamali.
 Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) Bw. Pascal Shelutete akimueleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel na kumuhakikishia ushirikiano wa kutosha katika eneo la mawasiliano lengo ni kufanya taarifa za Serikali zinawafikia wananchi.
 Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel akiwa katika Picha ya Pamoja na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbas pamoja na Viongozi wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO).
Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel mara baada ya kumaliza mazungumzo  25/09/2018 Mkoani Geita.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad