HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 26 September 2018

BENKI YA KILIMO TAYARI KUSAIDIA SAFARI YA KILOLO YA VIWANDA

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imesema ipo tayari kusaidia mapinduzi ya kilimo wilayani Kilolo mkoani Iringa kupitia ujenzi wa viwanda vya kimkakati vyenye kulenga kunyanyua maisha ya mkulima mdogo wilayani humo.

Ahadi hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine wakati akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe, Asia Abdallah aliyetembelea Makao Makuu ya Benki hiyo.

Bw. Justine amesema kuwa TADB ipo tayari kusaidia juhudiza wilaya ya Kilolo za kujenga kiwanda kisasa cha chai na mazao mengine ya kimkakati ili kuongeza kipato cha wakulima wilayani.

"Benki ipo tayari kutoa mtaji wa kujenga viwanda vya kimkakati ili kupata soko la mazao ya wakulima wadogo wadogo hasa wakulima wa chai," alisema.

Bw. Justine aliongeza kuwa Benki imelenga kutekeleza kwa vitendo dhana ya Tanzania ya Viwanda kwa kujielekeza katika uwekezaji wa viwanda vitakavyotoa ajira kwa vijana na wanawake wilayani humo.

Akieleza fursa zilizopo wilayani humo, Mkuu wa Wilaya, Mhe. Asia Abdallah alisema kuwa wilaya yake ina hekari zaidi ya 3,000 zilizotengwa kwaajili ya kilimo cha mazao ya kimkakati ikiwemo zao la chai.

"Tunafarijika kwa utayari wa Benki kusaidia uwekezaji wa kimkakati hasa katika ujenzi wa kiwanda cha chai wilaya kwetu," alisema.

Mheshimiwa Abdallah aliongeza kuwa wilaya ya kilolo ina fursa za kilimo ikiwemo uwepo wa ekari zaid ya 20,000 kwa ajii ya shughuli za kilimo cha mazao mbalimbali ikiwemo maparachichi, ufugaji wa samaki na nyuki.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kulia) akizungumza wakati Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe, Asia Abdallah (kushoto) alipotembelea Makao Makuu ya Benki hiyo kuzungumzia fursa mbalimbali za kilimo zilizopo wilayani Kilolo.
 Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe, Asia Abdallah (kushoto) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na uongozi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB). Anayemsikiliza ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kulia).
Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB, Bw. Augustino Matutu Chacha akizungumza wakati wa kikao hicho.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad