HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 30 August 2018

WAZAZI NA WALEZA SERENGETI WATAKIWA KUWA NA MGAWANYO SAWA WA MAJUKUMU YA KAZI KWA WATOTO WAO.

 Picha 1 ni Wanafunzi wa shule ya msingi Nyiberekera pamoja na shule ya msingi Nyamisingisi wakiwa katika maandamano kwa lengo la kufikisha ujumbe kupitia mabango mabalimbali waliyobeba kabla ya kuanza kwa Tamasha hilo.
 Wanafunzi wa shule ya msingi Nyamisingisi wakiimba wimbo ulibeaba ujumbe wa kupiga vita ukatili kwa watoto.
 Leah Kimaro ambaye ni mwezeshaji kutika shirika la RIGHT TO PLAY akitoa elimu juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia katika Tamasha hilo.
  Wanafunzi wa shule ya msingi Nyamisingisi wakiimba Shairi lenye ujumbe wa kupiga vita Ukatili.
 Wanafunzi wakionyesha Mchezo unaohusu stadi za maisha katika Tamasha hilo.
 Afisa Elimu kata ya Isenye Neema Fanuel akitoa msisitizo kwa wazazi na walezi kuendelea kutoa magawanyo sawa wa kazi katika familia.Na Frankius Cleophace Serengeti.
WAZAZI na walezi Wilayani Serengeti mkoani mara wametakiwa kuachana na suala la ubaguzi katika mgawanyo wa majukumu ya kazi majumbani ili kuleta usawa wa kijinsia huku mtoto wa kike akilimbikiziwa kazi nyingi kuliko mtoto wa kiume majumbani. 

Hayo yamebainishwa na wanafunzi katika tamasha la kutoa elimu juu ya masuala ya kupinga Mila na desturi zilizopitwa nawakati ukiwemo Ukeketaji, Ndoa za Utotoni pamoja na mimba za utoto tamasha lililoandaliwa na Shirika la RIGTH TO PLAY nakushirikisha shule za Msingi Nyamisingisi,Nyiberekera kata ya Isenye Wilayani Serengeti Mkoani Mara.

Elizabert Kirinda ni mwanafunzi wa shule ya msingi Nyamisingisi amesema kuwa majumbani watoto wa kike wamekuwa wakipewa kazi nyingi za kufanya kuliko watoto wa kiume jambo amabalo linachangia kukosa muda mwingi wa kijisomea wao kama mabinti hivyo wameomba wazazi na walezi kutoa mgawanyo sawa wa kazi ili kuondoa ubaguzi wa jinsia.

“Sisi wasichana majumbani tunapewa kazi nyingi kupika, kuchota maji kulea watoto na wavula hawafanyi kazi zozote na wakati mwingine tunachunga mifugo hatuna muda wa kusoma tukiwa nyumbani tunaomba wazazi waweze kugawanya sawa majukumu ya kazi majumbani” alisema Elizabert.

Leah Kimaro ambaye ni mwezeshaji kutoka shirika la RIGHT TO PLAY Wilayani Serengeti Mkoani Mara amezidi kuhimiza suala la jamii kutoa taarifa kwa wakati pale wanapoona watoto wanafanyiwa ukatili wa kijinsia na siyo kusubiri tukio kubwa kutokea.

Kimaro amesema kuwa shirikla hilo limekuwa likitoa elimu ya kupinga Mila a desturi ambazo zimepitwa na wakati kupitia michezo mbalimbali yakiwemo maigizo, ngonjera, nyimbo, shairi, maigizo pamoja na vichekesho lengo ni kufikisha ujumbe uliobeba masuala ya kupinga Mila na desturi zilizopitwa na waka tikatik jamii.

“Michezo hii tunafanya kwa kushirikisha wanafunzi pia watoto ambao wako nje ya shule pia kuna makocha ambao wanasaidia kuandaa watoto hawa ikiwemo suala la kutoa elimu ya kupiga vita ukatili wa kijnsia kwa watoto” alisema Kimaro.

Neena Fanuel ni Afisa elimu kata ya Isenye na Afisa Mtendaji wa kata ya hiyo Vicenti Kamuga wanazidi kusisitiza wazazi na walezi kuzingatia usawa katika mgawanyo wa kazi majumbani huku wakitaja baadhai ya ukatili ambao unafanyika katika jamii kuwa bado suala la ukeketaji linazidi kukumbatiwa na jamii licha ya jitiada za mashirika likiwemo shiria la RIGHT TO PLAY kuendekea kutoa elimu japo jamii inazidi kubadilikwa na kutoa taarifa pale wanapoona ukatili ukitendeka.

Shirika la RIGHT TO PLAY wamekuwa wakizunguka katika shule za misingi kwa kushirikisha watoto wa shule za msingi na sekondari pamoja ja jamii kwa ujumla na kutoa elimu ya kupiga vita ukatili kupitia michezo mablimba ili kubadili mitazamo hasi ya jamii katika wilaya ya Serengeti na kata kwenye baadhi ya kata.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad