HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 13 August 2018

TANZANIA YA PILI MICHEZO YA EAPCCO

 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akimkabidhi kombe la mshindi wa tatu nahodha wa timu ya mbio ya Polisi Tanzania wakati wa ufungaji wa Michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) iliyomalizika kwa Tanzania kushika nafasi ya pili kwa ujumla (Picha na Jeshi la Polisi).

Mwakilishi wa Jeshi la Polisi Rwanda akimkabidhi Kombe la mshindi wa Pili katika kulenga Shabaha Inspekta wa Polisi Tanzania wakati wa ufungaji wa Michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) iliyomalizika kwa Tanzania kushika nafasi ya pili kwa ujumla (Picha na Jeshi la Polisi).

Mkuu wa Jeshi la Polisi la Kenya akimkabidhi kombe la Ubingwa wa mpira wa miguu Inspekta Hashim Abdalah kutoka Tanzania wakati wa ufungaji wa Michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) iliyomalizika kwa Tanzania kushika nafasi ya pili kwa ujumla (Picha na Jeshi la Polisi).

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na Wanamichezo wa Polisi Tanzania wakati wa ufungaji wa Michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) iliyomalizika kwa Tanzania kushika nafasi ya pili kwa ujumla (Picha na Jeshi la Polisi).

Wanamichezo wa Polisi Tanzania walioshiriki Michezo ya Wakuu wa Majeshi ya Polisi ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) iliyomalizika kwa Tanzania kushika nafasi ya pili kwa ujumla wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa ufungaji wa michezo hiyo (Picha na Jeshi la Polisi).

Na. Jeshi la Polisi.
 Michezo ya Majeshi ya Polisi Ukanda wa Afrika Mashariki (EAPCCO) imemalizika Jijini Dar es Salaam huku Jeshi la Polisi nchini likishika nafasi ya pili katika ushindi wa jumla ambapo nafasi ya kwanza imeenda Kenya na  ya tatu Uganda.
Polisi Tanzania imeshika nafasi hiyo baada ya kuchukua jumla ya Medali 64, 15 za dhahabu, 25 za fedha na 24 za shaba huku Kenya ikiwa na medali 68, 25 dhahabu , fedha 20 na shaba 24.

Mshindi wa Tatu Uganda alijinyakulia Medali 36, Rwanda 27, Burundi nane, Sudani Kusini sita na Sudani moja  ambapo timu za Polisi Tanzania zimetwaa ubingwa katika  Soka, Mpira wa pete, Judo, na Kulenga Shabaha kwa upande wa Wanaume.

Akifunga Michezo hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi amewataka Wanamichezo hao kudumisha umoja na Amani katika mataifa wanayotoka ikiwemo kutumia michezo hiyo kubadilishana mbinu mbalimbali za kuzuia uhalifu.

Aliwapongeza Wanamichezo wote walioshiriki michezo hiyo kwa kuonyesha nidhamu na ushindani wa hali ya juu jambo ambalo limefanya michezo hiyo kuvutia watazamaji wengi.

 Kwa upande Wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amesema wanajipanga kimkakati ili kufanya vizuri zaidi katika Michezo ijayo ambayo inatarajiwa kufanyika nchini Kenya kwa kuwa ushindani ulikuwa mkubwa kutokana na nchi shiriki kujiandaa kwa muda mrefu.

“ Tumejifunza sana kupitia michezo hii hivyo tuliyojifunza tutayafanyia kazi ili kuhakikisha timu zetu zinafanya vizuri zaidi katika michezo hapa nchini na nje ya nchi ikiwemo kukaa kwa pamoja kwa muda mrefu badala ya kuingia kambini kwa muda mfupi” Alisema Sirro

Michezo inayoshindaniwa ni pamoja na soka ,mpira wa mikono, mpira wa wavu, mpira wa pete, Ngumi, Taekwondo, Judo na Riadha ambapo nchi zilizoshiriki ni pamoja na Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudani, Sudani Kusini na Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad