Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishirikiana na Madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Wafanyakazi wa Kiwanja cha Ndege cha Mwalimu Julius Nyerere kumshusha kutoka kwenye ndege Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alijeruhiwa katika ajali ya gari mkoani Manyara. Ndege hiyo iliwasili majira ya jioni katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishirikiana na
Madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,
Wafanyakazi wa Kiwanja cha Ndege cha Mwalimu Julius
Nyerere kumshusha kutoka kwenye ndege Waziri wa
Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye
alijeruhiwa katika ajali ya gari mkoani Manyara. Ndege
hiyo iliwasili majira ya jioni katika uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika uwanja
wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakati
akisubiri kumpokea Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.
Hamisi Kigwangalla ambaye alipata ajali ya gari mkoani
Manyara.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi
Kigwangalla akiwa ndani ya gari la wagonjwa kwa ajili ya
kupelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili
ya matibabu mara baada ya kuwasili katika uwanja wa
ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Ndege maalumu iliyombeba Waziri wa
Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye
alijeruhiwa katika ajali ya gari mkoani Manyara ikiwasili
katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere
kutokea mkoani Arusha majira ya jioni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
wanahabari mara baada ya kumpokea Waziri wa Maliasili
na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye alijeruhiwa
katika ajali ya gari mkoani Manyara.
No comments:
Post a Comment