HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 31 August 2018

NAIBU WAZIRI WA FEDHA AZINDUA DCB DIGITAL MJINI DODOMA

  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (wa tatu kushoto), akibonyezxa kitufe cha kompyuta kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma za kibenki katika mfumo wa kidigitali za Benki ya Biashara ya DCB jijini Dodoma. Wanaoangalia kutoka kushoto (mstari wa mbele ni; Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Godfrey Ndalahwa, Mwenyekiti wa Bodi ya DCB, Prof. Lucian Msambichaka, Mbunge wa Viti Maalumu, Mama Janeth Masaburi, Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Peter Pinda na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Patrobas Katambi. Huduma hizo ni pamoja na DCB Akaunti Kidigitali, Kibubu Kidigitali, Nusu Mshahara Kidigitali na huduma ya kutoa pesa katika ATM bila kadi.
 Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji akizungumza katika uzinduzi huo.
 Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda akizungumza katika hafla hiyo jijini Dodoma juzi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Godfrey Ndalahwa akikaribisha wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi huo jijini Dodoma.
 Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Peter Pinda (katikati), akishikana mikono na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashaitu huku Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Biashara ya DCB, Prof. Lucian Msambichaka akiangaalia mara baada ya uzinduzi huo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya DCB, Prof. Lucian Msambichaka (kulia), akikabidhi tuzo kwa Naibu Waziri wa Fedha, Dk. Ashatu Kijaji aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo jijini Dodoma
Baadhi ya waalikwa waliohudhuria tukio la uzinduzi wa DCB Digital jijini Dodoma.
                            
Na mwandishi wetu,Globu ya Jamii
BENKI ya Biashara ya DCB imezindua huduma maalum ijulikanayo kama DCB DIGITAL BANKING ambayo ni huduma za kibenki zinazopatikana kwa njia ya simu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Jijini Dodoma Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dk Ashatu Kijaji alisema sote tumesikia DCB walikua wakwanza kuorodheshwa kwenye soko la hisa na leo DCB inakwenda kidijitali na ni ya kwanza kuzindua bidhaa zake nne muhimu hili ni jambo zuri sana kwa Benki ya DCB na Taifa letu hongereni sana.

Amesema ‘’Napenda pia niwashukuru sana uongozi wa benki hii kwa kutupatia nafasi sisi Wizara ya Fedha na Mipango kuja kua sehemu ya kihistoria katika sekta yetu ya fedha”.

Nikiwa kama kiongozi wa kusimamia maswala ya fedha nimefarijika sana kuwa pamoja nanyi lakini pia nimefarijika zaidi baada ya kuisikia historia ya DCB ikielezwa hapa mbele yetu na viongozi wa benki hio. Kwakweli ni tukio muhimu sana kwetu sekta ya fedha kwasababu kwa kauli mbiu hii ya SIMU YAKO,TAWI LETU inamaana Benki inawafikia watanzania kule walipo.

Kutokana na Ripoti ya Finscope ya mwaka 2017 ilionyesha idadi ya watanzania waliojiunga na mfumo rasmi wa kifedha imeongezeka kwa asilimia 14 kutoka mwaka 2013 chachu ya ongezeko hili ni pamoja na urahisi wa upatikanaji wa huduma za kifedha kupitia simu zetu za mkononi na mashine za kutolea fedha. Lakini kutokana na uzinduzi huu wa leo naamini tutaongeza zaidi ya asilimia 70 kwasababu tutawafikia kule waliko.

Nawaelekeza DCB kuwatembelea wakulima wetu kwa sababu moja ya mpango wa serikali wa maendeleo wa miaka mitano ulioanza kutekelezwa tangu 2016 hadi 2021 umejikita zaidi katika kujenga uchumi wa viwanda, hivyo hakuna Viwanda bila taasisi za kifedha hususan benki zetu na hakuna uchumi wa Viwanda bila wakulima ambao ndio wazalishaji wa malighafi za viwanda. Kupitia huduma kama hizi za kibenki nawahakikishia tutaifikisha Tanzania yetu ya uchumi wa kati wa viwanda kabla ya mwaka 2015.

Ninachoomba elimu ya kifedha ambayo mmeitoa kwa wajasiriamali wa Dar es salaam nendeni mkaitoe kwa wakulima na wafugaji wa Tanzania kwani serikali inakwenda kuhakikisha Mkulima anapata soko la mazao yake.

Ameongeza Serikali yetu ya awamu ya tano ambayo ipo chini ya Muheshimiwa Rais John Pombe Magufuli inatambua wazi mchango wa sekta ya fedha hususan benki zetu katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na kufikia malengo ya Taifa letu hivyo endeleeni kuwekeza lakini pia kubuni bidhaa na huduma zinazo lingana na mazingira ya watanzania na serikali kwa upande wetu tutaendela kuhakikisha mazingira ya uwekezaji yanaendelea kuwa bora.

Kuendelea kuboresha huduma za kibenki, mwezi huu wa nane mwaka 2018 Serikali imechukua hatua madhubuti za kiutawala na kisera ambazo ningependa kuisema leo hapa kwa mara ya kwanza ni kushusha riba kutoka asilimia 16 hadi asilimia 8.

Hivyo upatikanaji wa fedha utakua ni rahisi kwa mabenki yetu.Hii yote ni kuhakikisha watanzania wanapata mitaji kwa gharama nafuu, wito wangu kwa mabenki yote ikiwemo Benki yetu ya DCB kuakisi jitihada hizi za serikali yenu ya awamu ya tano.

Dk Kijaji ameongeza “Nimefarijika sana kusikia kuwa DCB ni moja ya benki chache zilizojiunga na mfumo wa serikali ujulikanao kama Government e Payment Gateaway (GePG ) ambao ni mfumo wa serikali unaotumika kufanya malipo mbalimbali hivyo kupanua wigo wa malipo ya serikali”.

Mwenyekiti wa Bodi ya DCB Profesa Lucian Msambichaka ameongeza ‘’ Benki imeendelea kuimarika na Mwezi uliopita Benki imetangaza kupata faida katika kipindi cha nusu ya kwaka kilichoishia mwezi Juni mwaka 2018, mafanikio haya yametokana na ubunifu wa bidhaa zinazokidhi mahitaji ya wateja wetu, uweledi na huduma bora alisema.

Mkurugenzi Mkuu wa DCB Ndugu Godfrey Ndalahwa nae amesema DCB itaendelea kutoa huduma bora na za ubunifu ili kuweza kushindana kwenye soko. Bidhaa zetu ni nzuri sana na zenye ubunifu mkubwa. Kupitia DCB Digital mteja sasa ataweza kufungua akaunti ya muda maalum (Digital FDR) , Akaunti ya malengo (Kibubu Digital Account) ,Digital Salary advance na vilevile sasa anaweza kupata huduma za kutoa pesa kwenye ATM za umoja switch zilizoenea nchi nzima bila kutumia kadi ya benki (Cardless ATM).

Kwa Mawasiliano:
Rahma Ngassa
Mkuu wa kitengo cha Masoko
Simu Namba: +255 22217201

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad