HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 14, 2018

Mradi wa kutoa elimu ya matumizi ya mitandao kwa wanawake waanzishwa

Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Women at Web Tanzania imezindua mradi maalumu wenye lengo la kutoa mafunzo ya matumizi ya mitandao ili kuongeza uwepo wa kundi hili mitandaoni.

Mradi huo unaofadhiliwa na Shirika la DW Akademie la nchini Ujerumani una lengo la kuhamasisha matumizi bora ya mitandao ikiwamo kuongeza  mijadala ya maendeleo kwa wanawake katika mitandao.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi huo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam, mmoja wa viongozi wa mradi huo Carol Ndosi amesema kwamba moja ya shughuli zitakazofanyika katika uhamasishaji huo ni mafunzo kwa wanawake yanayohusu njia za kujilinda na vurugu za mitandao, kutambua fursa zilizopo mitandaoni pamoja na mambo mengine.

Alisema kuwa kwa sasa Tanzania hakuna takwimu zilizo wazi za udhalilishaji wa wanawake kwenye mitandao japokuwa wengi waliopo wameshakutana na aina ya udhalilishaji kwenye mitandao, hasa ya kijamii.
“Idadi ya watu wanaomiliki smart phone inaongezeka hivyo kuongeza hatari za wanawake kuwa wahanga wa unyanyasi katika platform hizo, kwa hiyo kupitia mradi huu, pamoja na kuhamasisha wanawake kuongezeka kutumia hii mitandao, tutawapatia mafunzo ya namna ya kujilinda ama kutambua wale wanataka kuwafanyia ukatili.

“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa kwa kuwa bado tuna ‘gap’ kubwa sana la wanawake kushiriki katika mijadala ya maendeleo nje ya mitandao, basi watumie fursa za mitandao kushiriki mijadala hiyo na kujiletea maendeleo,” alisema Ndosi.
Kwa kuanzia, mradi huo utaendesha mafunzo katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na pia kwa upande wa Zanzibar.






No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad