HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, August 25, 2018

MAAFISA UHAMIAJI MAKAO MAKUU WAFANYA USAFI MAKAZI YA WAZEE NUNGE-KIGAMBONI.




MAAFISA uhamiaji wamefanya usafi katika makazi ya wazee, watu wenye ulemave na wasiojiweza kilichopo wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam leo pamoja na kuwapa zawadi mbalimbali ikiwa ni kwaajili ya kuwafariji.

Zawadi walizowadawadia ni pamoja na Mchele,maharage, sukari, unga, mafuta, sabuni na sementi.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala akizungumza walipowatembelea wazee hao leo amesema kuwa sementi waliyopewa ni kwaajili ya kutengenezea uzio wa eneo la kulima mboga mboga kwaajili ya wakazi wa makazi hayo.

Nae Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Rahel Mhando amewasihi watunze mazingira yao pamoja na mazingira ya vyoo pia amewaomba wataalamu wa saikolojia waweze kuwapa wakazi wa makazi ya Nunge ili kuwaweka katika usawa wa kimawazo kwani wengi wao hawana ndugu.

Kwa upande wa mwakilishi wa wakazi wa makazi ya Nunge yaliyopo wilya ya Kingamboni, Salumu Ubwabwa amewashukuru Maafisa uhamiaji kwa kuwafariji pamoja na kwapa msaada wa vitu mbalimbali.

Ubwabwa amesema kuwa changamoto zinazowakabiri ni pamoja na kukosa uzio wa eneo lao,umeme na maji kwa baadhi ya makazi pamoja na geti la kuingilia katika makazi hayo.

Pia amewaomba watu mbalimbali wanaoweza kuwasaidia waweze kuwasaidi kwani wao niwazee na hawawezi kujitafutia wenyewe chakula.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni Rahel Mhando akizungumza na kuwakaribisha maafisa na watumishi wa uhamiaji makao makuu walipotembelea katika Makazi ya wazee, watu wenye ulemave na wasiojiweza kilichopo wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam leo Augusti 25,2018.
 Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala kulia akifanya usafi leo Augusti 25,2018 katika Makazi ya wazee, watu wenye ulemave na wasiojiweza kilichopo wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam mara baada ya maafisa uhamiaji kutembelea katika makazi yao.
 walipotembelea katika Makazi ya wazee, watu wenye ulemave na wasiojiweza kilichopo wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam leo Augusti 25,2018.
  
 Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala kulia na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni Rahel Mhando kushoto wakifyeka majani pamoja na miti ambayo ipo katika eneo la makazi ya  wazee, watu wenye ulemave na wasiojiweza kilichopo wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam leo Augusti 25,2018 walipotembelea leo kwaajili ya kufanya usafi pamoja na kuwafariji watu hao waliopo katika kituo hicho.

  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala akifyeka eneo la  Makazi ya wazee, watu wenye ulemave na wasiojiweza kilichopo wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam leo Augusti 25,2018 walipotembelea leo kwaajili ya kuwafariji na kuwapa zawadi mbalimbali.
 Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala kulia akiwa kwenye picha na Mzee asiyeona pamoja na wajukuu zake.
 Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala akioneshwa nyumba ambazo watu wa kituo cha Nunge wakiishi.
 Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala akimsaidia bibi kushuka chika wakati walipotembelea kituo cha Nunge wilaya ya Kigamboni leo.
 Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala kulia akisafisha nyumba ya bibi Mgogo iliyopo katika makazi ya wazee, watu wenye ulemavu na wasiojiweza Nunge Wilaya ya Kigamboni leo Augusti 25,2018.

 Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni Rahel Mhando wakiwa jikoni kujionea mlo kamili wanaopewa watu wanaoishi katika Makazi ya wazee, watu wenye ulemave na wasiojiweza kilichopo wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam leo Augusti 25,2018.

Mzee wa burudani katika Makazi ya wazee, watu wenye ulemave na wasiojiweza kilichopo wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam leo Augusti 25,2018 akipiga gita mara baada ya maafisa uhamiaji makao makuu kutembelea leo katika makazi yao. 
  Picha ya pamoja.
  Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala akizungumza na wazee waliofika wa makazi ya wazee, watu wenye ulemavu na wasiojiweza wa Nunge leo mara baada ya maafisa Uhamiaji Makao Makuu kufika katika kituo hicho na kuwafariji.
  
 Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala akitoa zawadi kwa wazee wa kituo cha Nunge kilichopo wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam leo Augusti 25,2018.
Mzee Salumu Ubwabwa akiwashukuru maafisa uhamiaji waliofika kuwafariji, kuwafanyia usafi pamoja na kuwapa zawadi mbalimbali katika makazi ya wazee, watu wenye ulemavu na wasiojiweza cha Nunge kilichopo wilya ya Kingamboni jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad