HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 26 August 2018

KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE ZA LAAC NA PAC ZAENDELEA NA VIKAO VYAKE BUNGENI MJINI DODOMA

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Mbunge wa Kilwa kaskazini, Mhe. Vedasto Ngombale Mwiru (katikati) akisisitiza jambo wakati Kamati hiyo ikipokea taarifa ya maagizo ya kamati na Mapendekezo ya taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu Hesabu za Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017. Kikao kilichofanyika leo Bungeni Jijini Dodoma
Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mhe. Mwigulu Nchemba akizungumza pale kamati hiyo ilipokutana na Mwenyekiti na Menejimenti ya Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWSA) wakati wa kupokea na kujadili taarifa ya CAG kuhusu Hesabu za Mamlaka Kwa Mwaka wa Fedha ulioishia 2016/2017. Kikao kilichofanyika leo Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Mjumbe na Mbunge wa kiwani, Mhe. Abdallah Haji Ali
Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na Mbunge wa Kilindi, Mhe. Omari Kigua akizungumza pale kamati hiyo ilipokutana na Mwenyekiti na Menejimenti ya Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWSA) wakati wa kupokea na kujadili taarifa ya CAG kuhusu Hesabu za Mamlaka Kwa Mwaka wa Fedha ulioishia 2016/2017. kikao kilichofanyika leo Bungeni Jijini Dodoma.
Mkurugenzi  wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, Ndg. Revocatus Kiuuli akizungumza na Wajumbe wa  kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) (hawapo kwenye picha) wakati wa kuwasilisha taarifa ya maagizo ya kamati na Mapendekezo ya taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Hesabu za Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 kikao kilichofanyika leo Bungeni Jijini Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Tauhida Nyimbo (katikati) akizungumza wakati Kamati hiyo ikipokea taarifa ya maagizo ya kamati na Mapendekezo ya taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Hesabu za Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 kikao kilichofanyika leo Bungeni Jijini Dodoma. Kushoto ni Mjumbe na Mbunge wa Bukene Mhe. Selemani Zedi
(PICHA NA DEONISIUS SIMBA - OFISI YA BUNGE)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad