HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, August 29, 2018

JWTZ KUTIMIZA MIAKA 54 SEPTEMBA 1, LAHIMIZA WANANCHI KUSHIRIKI KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA

Na Angess Francis Blogu ya Jamii

WATANZANIA wametakiwa kujitokeza na kushiriki kwa wingi katika kufanya shughuli za usafi wakati maadhimisho ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) kutimiza miaka 54 tangu kuanzishwa kwake.

JWTZ linatarajia kufikisha miaka 54 ifikapo Septemba 1 mwaka huu.Jeshi hilo lolianzishwa mwaka 1964.
Akizungumzia sherehe hizo Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano  wa JWTZ Kanali Ramadhani Dogoli amesema katika maadhimisho hayo ya mwaka huu jeshi limeanza kufanya  shughuli mbalimbali za kijamii  pamoja na kujishughulisha katika michezo.

“Itakumbukwa kila mwaka  inapofika tarehe hiyo bada ya kubadilishwa  jina kutoka Tanganyika Rifle (TR)  kuwa Jeshi la Ulinzi  la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

"Na sherehe hizo kila mwaka tumekuwa tukifanya shughuli za kijamii kwa kufanya usafi  kwenye maeneo ya kambi zote za jeshi na kushiriki katika michezo,”amesema.
Amefafanua michezo inayoendelea kuchezwa ni mpira wa miguu,Pete,wavu, golf na mingine na kwamba timu za jeshi na za uraiani ndizo zinashiriki michezo hiyo.
Kanali Dogoli amefafanua shughuli hizo zilianza kufanyika  Agosti 27  mwaka huu na kwamba zitaendelea hadi siku kilele cha sherehe hizo.

Hivyo limesisitiza umuhimu wa watanzania wote wenye mapenzi mema kungana kuadhimisha siku  hiyo kwa kujitokeza kufanya usafi katika maeneo yao wanayoishi na  kuyaweka katika hali ya usafi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad