HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 13 August 2018

Jacqueline Mengi apata tuzo ya ujasiriamali wa mwaka

Na Mwandishi wetu
Mfanyabiashara wa Samani anayeinukia kwa kasi nchini Jacqueline Mengi amenyakua tuzo za biashara za Stevie ya Mjasiriamali wa mwaka kategori ya uzalishaji kupitia kampuni yake ya Amorette Ltd.
Katika tuzo hizo sehemu ya uzalishaji (Manufacturing), tuzo ya dhahabu ya mjasiriamali ilienda kwa watengenezaji wa lishe Hauppauge, New York Marekani na ilienda kwa Jason Provenzano, ambaye ni mwasisi na ofisa mtendaji mkuu wake.
Jacqueline Mengi atakabidhiwa tuzo hiyo Oktoba 20 mwaka huu mjini London, Uingereza.
Tuzo za dhahabu, fedha na shaba zinatolewa baada ya ushindani mkali miongoni mwa washiriki 3,900 kutoka taasisi na watu binafsi wa mataifa zaidi ya 74.
Hizi ni tuzo za kimataifa zinazotolewa katika madaraja mbalimbali ya menejimenti, kampuni, masoko, mahusiano, huduma za kijamii, ujasiriamali, utoaji wa bidhaa mpya, bidhaa mpya za tehama, tuzo kwa tovuti na zaidi.
Zaidi ya watendaji 270 duniani kote walishiriki katika kuwania tuzo hizi wakifanyiwa tathmini na majaji 12.
Jacqueline Mengi ambaye ndiye Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Amorette akizungumzia ushindi wake alisema amefurahishwa na ushindi huo ikionesha kwamba mchango wake duniani unatambuliwa.
Amorette ni kampuni ya kutengeneza samani zinazotokana na mbao zinazopatikani nchini Tanzania ikiwemo miti migumu.
Samani zinazotengenezwa huangaliwa kwa undani ili kukamilisha umaridadi wa samani. Yeye pamoja na kuwa balozi wa WildAid na akiwa ndani ya bodi kadhaa; mama wa watoto pacha wavulana; mke kwa mfanyabiashara mwenye mafanikio makubwa na akiendesha taasisi ya hisani ya elimu), Jacqueline huhakikisha anakagua kila samani inayozalishwa kiwandani kwake kabla ya kuuzwa au kusafirishwa.
Jacqueline, mzaliwa wa Tanzania, aliyefunzwa kubuni uzuri wa ndani, ni mwanzilishi na mbunifu mkuu wa Molocaho by Amorette, kampuni ya Tanzania inayojishughulisha na utengenezaji wa samani bora kwa namna mteja anavyohitaji, samani, nyuzi, taa, urembaji, samani za nje na kwenye bustani.
Molocaho, moja ya makampuni ya Afrika Mashariki ya samani yanayokua kwa kasi, imejipatia nafasi kubwa ya heshima kwa kuhakikisha kwamba inatumia mali ghafi na mbao njema pekee za Tanzania kutengeneza samani zenye kwenda kimataifa.
Jacqueline Mengi ni mojawapo ya watu wanaotambulika kirahisi kabisa nchini Tanzania. Mwaka 2000 alishinda taji la urembo la Miss Tanzania na kuiwakilisha Tanzania katika shindano la urimbwende la dunia (Miss World). Baada ya muda alipata heshima ya kuwa mmoja wa wanamuziki mahiri na kuweza kutoa nyimbo kadhaa zilizoshika chati Afrika Mashariki.
Pamoja na kuwa mrimbwende na mwanamuziki anasema mapenzi yake makubwa ni ubunifu wa uzuri wa ndani wa nyumba.
Kwa tuzo hiyo inadhihirisha kwamba Amorette ni chata ya kuaminika yenye mafanikio makubwa miongoni mwa watu wa daraja la juu nchini Tanzania.
Amorette, kampuni inayoshughulika na ubunifu wa masuala ya ndani ilianzisha programu ya kusimamia mafunzo kwa mafundi wa hapa Tanzania kuwafanya mafundi wa Tanzania kufikia uwezo wa kubuni na kutengeneza bidhaa zenye hadhi ya kimataifa.
Miongoni mwa waliotwaa tuzo hizo za dhahabu ni Telkom Indonesia zikiwa 14; Switching-Time, China ( sita); ASDA’A BCW, Falme za Kiarabu (tano); Makers Nutrition, USA (tano); PJ Lhuillier, Inc, Philippines (tano); na Reklam5 Digital Agency, Turkey (tano). Walionyakua tuzo nne za dhahabu za Stevie ni pamoja Akbank, Uturuki; Cisco, worldwide; FIS,Marekani; GXEVER, China; Jeunesse Global, Marekani; LLORENTE & CUENCA, Hispania; Magnet20, Uturuki; Ooredoo Group, worldwide; PT Petrokimia Gresik, Indonesia; Ribose, Hong Kong; Thai Life Insurance, Thailand; Turk Telekom, Uturuki; na Yapi Kredi Bank, Uturuki.
DHL Express, worldwide, ina tuzo 46 za dhahabu,fedha na shaba. Waliochukua tuzo nane au zaidi za Stevie ni pamoja na CROWDCONSULTANTS 360 Gmbh, Ujerumani; Manila Electric Company, Philippines; Marco de ComunicaciĆ³n, Hispania; Port It Global, Kenya; Sahibinden.com, Uturuki; Thai Life Insurance, Thailand; Twenty Twenty Media Pvt. Ltd, India; na Vakifbank, Uturuki.
Nchi tano ambazo zina washindi wengi katika tuzo hizo ni Marekani, Uturuki, Korea Kusini , Uingereza na Indonesia.
Tuzo za Stevie zilianzishwa mwaka 2002 na toka wakati huo zimeshatolewa kwa watu mbalimbali katika nchi zaidi ya 60.
Mwaka 2012 tuzo hizo zikitimiza miaka kumi, ilianzishwa kategori ya fedha na shaba badala ya ile moja ya Dhahabu. Mwaka 2013 kulianzishwa tuzo kuu ya Stevie (Grand Stevie Award trophy) ambayo hutolewa kwa taasisi chache katika kila maeneo sita ya ushindani.
Katika kila tuzo za Stevie kila anayeingia nafasi ya kwanza anakuwa na tuzo ya dhahabu na wale watakaokuwa na alama angalau 8.0 na alama pengine 10 wataingia katika mkumbo wa kupata tuzo ya fedha na waliofikia fainali wote chini ya hapo watapatiwa tuzo ya shaba.
Kuhusu tuzo za Stevie
Jina Stevie linatokana na jina Stephen, linalotokana na neno la kigiriki na maana yake ni taji.
Tuzo ya Grand Stevie ina urefu wa inchi 16 imetengenezwa kwa mkono na ina karat 24 ya dhahabu.
Orodha kamili za washindi kwa tuzo za Stevie unaweza kusoma www.StevieAwards.com/IBA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad