HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 20, 2018

AMANA BENKI IMEANZA KUTOA HUDUMA KWA WATEJA KUPITIA WHATSAPP

Amana Benki inaendelea kujivunia kuwa benki ya kwanza Tanzania inayoendeshwa kwa kuzingatia misingi ya kiislamu, yenye malengo ya kutoa huduma za kibenki za kisasa na za kipekee, kwa njia iliyowazi na kwa kutumia teknolojia ya kisasa kwa manufaa ya wateja na wadau wote. Amana Benki kwa takribani miaka saba sasa imekuwa kwa kasi huku ikihudumia watu wote bila kubagua dini zao.

Katika kurahisisha kutoa huduma za kibenki kwa wateja, Amana Bank imekuwa ikiwafikia wateja kwa njia mbalimbali ikiwemo matawi yake, mawakala, huduma za kibenki kupitia simu ya mkononi na intaneti na hata ikibidi kuwafata wateja mahali walipo.

Kwa mujibu wa benki hiyo mnamo mapema mwezi Agosti,imezindua rasmi njia rahisi ya mawasiliano na wateja wake kwa kutumia mfumo mpya wa njia ya simu maarufu kwa jina la Whatsapp.

Kwa sasa wateja wa benki hiyo na watu wote kwa ujumla wanaweza kutumia programu ya simu ya mkononi maarufu kwa jina la Whatsapp kupata huduma moja kwa moja kutoka kitengo cha huduma kwa wateja kupitia namba 0657 980 000.

Akizungumza ofisini kwake Mkurugenzi Mtendaji wa Amana Benki Dkt Muhsin Salim Masoud alisema kuwa “tumeshawishika kuanza kutumia mtandao wa WhatsApp katika kitengo chetu cha huduma kwa wateja ili kwenda sambamba na matumizi ya teknolojia ya mawasiliano katika kuboresha huduma kwa wateja wetu,  matumizi ya WhatsApp yatawezesha wateja wetu kuwasiliana na kitengo chetu cha huduma kwa wateja hata wakiwa nje ya nchi au mahali popote ambapo hawawezi kupiga simu ya kawaida”. Aliongeza kuwa kwa sasa matumizi ya mawasiliano kwa njia ya WhatsApp na Intaneti kwa ujumla yameshika kasi kubwa hivyo ni busara kutumia njia hii ilikuwapa fursa na urahisi watu na wateja wenye kumudu kutumia njia hii kupata huduma kwa wepesi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Amana Bank, Dk. Muhsin Salim Masoud akizungumza jambo wakati akizungumzia huduma ya mtandao wa WhatsApp katika kitengo cha huduma kwa wateja ili kwenda sambamba na matumizi ya teknolojia ya mawasiliano katika kuboresha huduma kwa wateja.

Teknolojia inakua kwa kasi sana na wateja sasahivi wanahitaji njia mbadala na rahisi ili waweze kuwasiliana na kupata taarifa za kibenki kwa muda wowote. Hii ndio sababu inayotusukuma kubuni namna ya kurahisisha njia zetu za mawasiliano na wateja popote pale walipo”, alisema Kaimu Meneja Mkuu wa Biashara Bw. Dassu Mussa.

Njia hii itawawezesha watu wote wanaotumia simu pendwa (smart phone) zilizomo katika mfumo wa IOS na Android kuweza kupata huduma mara moja bila ulazima wa kufika katika matawi ya Amana Benki.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa Amana Benki ametoa rai kwa watu kutumia njia hii ya mawasiliano vizuri ili kupata huduma kwa wakati na ameahidi kuwa Amana Benki itaendelea kutoa huduma bora za kibenki kwa kuzingatia matumizi ya teknolojia ya kisasa kwa manufaa ya wadau wote.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad