Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Utalii, Jaji Mstaafu, Thomas Mihayo ( wa tano kulia) akiwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Deograsius Mdamu ( wa sita kushoto) wakiwa na Baadhi ya Waoneshaji wakifurahia ushindi wa Tuzo katika banda la Wizara ya Maliasili na Utalii. Tuzo hizo ni mshindi wa kwanza katika kipengele maalum cha Best Export Products Exhibitors na Mshindi wa pili katika kipengele cha Trade in Services katika Maonesho hayo. Tuzo hizo zilikabidhiwa jana na Waziri Mkuu wa Jahuri ya Muungano wa Tanzania. Majaliwa Kassim Majaliwa katika viwanja vya Sabasaba. ( Picha na Lusungu Helela-MNRT)
Baadhi ya Waoneshaji wakifurahi ushindi wa Tuzo walizokabidhiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassimu Majaliwa katika banda la Wizara ya Maliasili na Utalii, Wa kwanza kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Deograsius Mdamu.
Muonekano mpya wa Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii sehemu ya mapokezi katika Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimtaifa ya Dar es Salaam .Banda la Wizara limekuwa miongoni mwa mabanda yenye mvuto wa kipekee kutokana na utofauti wake wa uwepo wa wanyamapori hai kama vile Simba, Chui , Chatu, Nyati, ndege wa aina mbalimbali na wale watakaopenda kuona wanyamapori hao kiingilio ni shilingi 1,000 kwa watu wazima na 500 kwa watoto wadogo. ( Picha na Lusungu Helela-MNRT)
aswira za tuzo hizo
Baadhi ya Waoneshaji wakifurahi ushindi wa Tuzo walizokabidhiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Majaliwa Kassimu Majaliwa katika banda la Wizara ya Maliasili na Utalii.
No comments:
Post a Comment