HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, 5 July 2018

Airtel yazindua Hakatwi MTU HAPA –Tuma Pesa Bure kupitia Airtel Money

Kampuni ya simu za mkononi inayoongoza kwa utoaji wa huduma bora za Smartphone Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Airtel Money leo imetangaza na kuzindua huduma mpya kwa wateja wote wanaotumia huduma ya kutuma na kupokea pesa kupitia Airtel Money kwa sasa wataweza kutuma na kupokea pesa bure bila ya makato yoyote.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam kwa niamba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Isack Nchunda alisema, “Tunayo furaha kubwa kuona ungezeko la watumiaji wa Airtel Money kila siku, tunaamini ya kuwa malengo ya serikali ya kuhakikisha inafanikisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa kila mwananchi linaelekea kupata mafanikio makubwa. Leo Airtel tunazindua huduma hii inayojulikana kama HAKATWI MTU HAPA – Tuma Pesa Bure ili kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali na kuwawezesha wateja wetu zaidi ya milioni 10 nchini kuweza kutuma na kupokea Pesa BURE”.

“Mwaka jana Airtel tulizindua huduma ya ya kutuma na kupokea pesa bure kwa wateja wa Airtel Money wanaotuma pesa kuanzia 200,000 na kuendelea. Tumezingatia tena uhitaji wa wateja wetu wengi hivyo kupitia HAKATWI MTU-Tuma Pesa Bure tunaamini wale wanaotuma pesa chini ya hapo wataweza kufurahia huduma hii ya Bure.

 Ni imani yetu kwamba huduma ya tuma na pokea pesa bure kupitia Airtel Money itakuwa ni chachu kwa wale ambao sio wateja wa Airtel Money kuanza kutumia huduma hii salama, rahisi na ya uhakika,  Tunategemea kuona wateja wakichangamkia  Fursa hii ya kutuma na kupokea pesa bila makato yoyote ili  kuokoa pesa  hadi Sh 5,000 kuanzia sasa”. alieleza Nchunda

Nchunda aliongeza kuwa “Airtel tumejiwekea mikakati ya kuendeleza huduma bora nchini kote kwakuongeza Idadi ya mawakala wetu na sasa tunao wakala zaidi ya elfu 55. Tunaendelea kuongeza mawakala kupitia usambazaji wa vioski vya Airtel Money na kuongeza Maduka ya Airtel Money Branch ambayo sasa tayari yanatoa huduma kama wakala wa kawaida  na pia kama wakala mkubwa ambapo hadi sasa hivi tumeshafungua matawi (Airtel Money Branch) zaidi ya 300 yanayotoa wigo mkubwa zaidi wa mawakala nchini. Ni imani  yetu tutaendelea kuwafikia wateja wengi zaidi kwa kutumia huduma hii ya Hakatwi MTU HAPA – Tuma Pesa Bure. Ili mteja kuweza kufurahia huduma hii ya Hakatwi MTU HAPA, atatakiwa kupiga *150*60# na kuchangua Tuma pesa bure.”

Nchunda alisema kuwa Airtel inalenga zaidi katka maboresho ya huduma za kifedha hapa nchini kwa kuwafikia Watanzania zaidi ya 80% ambao bado hawajafikiwa na huduma za kibenki.  Aliongeza kuwa Airtel itaendelea kuleta ubunifu mbalimbali wa wahuduma zenye suluhisho kwa jamii kupitia Airtel Money ambazo ni rahisi na hakika ikiwemo huduma pekee ya kutoa mikopo binafsi kwa wateja kupitia simu ya mkononi yaani Timiza Loans na Timiza Vicoba maalum kwa mikopo ya vikundi. 

Vilele Airtel Money inawezesha malipo mbalimbali yakiwemo  yale ya humuma za  serikali ( e-government) ambayo wateja wanaweza kufanya hayo malipo popote kwa wakati mmoja. “Pia huduma ya Airtel Money imeunganishwa na mabenki zaidi ya 40 nchini ili kurahishishia wateja kufanya miamala mbali mbali kama vile kuhamisha pesa kutoka kwenye akaunti ya benki na kutuma kwenye akaunti ya Airtel Money muda wowote na sehemu yeyote ile”.
Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchunda akiongea wakati wa kuzindua huduma inayojulikana kama HAKATWI MTU HAPA – Tuma Pesa Bure ambapo wateja wote wanaotumia huduma ya kutuma na kupokea pesa kupitia Airtel Money kwa sasa wataweza kutuma na kupokea pesa bure bila ya makato yoyote kwa kupinga *150*60# kisha changua tuma pesa bure.
Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano akiongea wakati wa kuzindua huduma inayojulikana kama HAKATWI MTU HAPA – Tuma Pesa Bure ambapo wateja wote wanaotumia huduma ya kutuma na kupokea pesa kupitia Airtel Money kwa sasa wataweza kutuma na kupokea pesa bure bila ya makato yoyote kwa kupinga *150*60# kisha changua tuma pesa bure.
Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchunda – kulia na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni wakionyesha bango baada kuzindua huduma inayojulikana kama HAKATWI MTU HAPA – Tuma Pesa Bure ambapo wateja wote wanaotumia huduma ya kutuma na kupokea pesa kupitia Airtel Money kwa sasa wataweza kutuma na kupokea pesa bure bila ya makato yoyote kwa kupinga *150*60# kisha changua tuma pesa bure.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad