HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 12 July 2018

WASHINDI WA AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY DROO YA TATU WAPATIKANA

Mkazi wa Morogoro, Frank Kisayo ameshinda zawadi ya televisheni ya kisasa aina ya Samsung yenye ukubwa wa inchi 32 kupitia promosheni ya Amsha Amsha Ushinde na Airtel Money ambayo inaendeshwa kampuni ya simu ya Airtel Tanzania na kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa.

Kisayo ambaye ni mkulima, alishinda televisheni hiyo kwenye droo ya tatu iliyofanyika kwenye Ofisi Makao Makuu ya Ofisi za kampuni ya simu ya Airtel jijini.

Akizungumza kwa njia ya simu mara baada kushinda droo hiyo, Kisayo alisema kuwa amefurahi sana kushinda zawadi hiyo yenye thamani si chini ya Sh750,000.

“Siamini kama nimeshinda, nasubiri kwa hamu zawadi yangu, naamini sasa suala la kununua televisheni kwangu limeisha baada ya kushinda zawadi hii nono ya droo ya Amsha Amsha,” alisema Kisayo.

Mbali ya Kisayo, pia Masoud Saleh wa Kisarawe  na Shadrack Sanga wa Manyara kila mmoja alishinda simu ya mkononi aina ya Samsung Galaxy yenye thamani Sh500,000.

Pia Eric  Samwel ambaye ni mkazi wa Tanga alijishindia jezi na tiketi ya msimu ya kuona mechi ya Yanga na Simba za msimu ujao.

Maneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando alisema kuwa mpaka sasa washindi watatu wa televisheni, simu 25 na jezi 25 wamepatikana katika droo hiyo.

“Bado televisheni moja, simu tano na jezi za Yanga na Simba tano ambazo zitatolewa katika droo ya mwisho ya promosheni , tunawaomba wateja wetu kuendelea kubeti kupitia Airtel Money na SportPesa Limited,” alisema Mmbando.

Meneja Uhusiano wa Kampuni ya SportPesa, Sabrina Msuya alisema kuwa promosheni hiyo imeshika kasi na wateja wengi wa Airtel Money na SportPesa wameweza kubadili maisha yao kwa kushinda zawadi nono.

Sabrina alisema kuwa wameamua kuendesha promosheni hiyo ili kuwazawadia wateja wao na kuwaomba washiriki ili waweze kufaidika.

 Alisema kuwa bado droo moja ya kuwazadia washindi wa promosheni hiyo ambayo inafanyika nchi nzima. Washindi wa mikoani watachukua zawadi zao kupia maduka ya kampuni ya Airtel husika.
Meneja Matukio wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Dangio Kaniki akiongea na moja ya washindi wa AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY kwa kushirikiana na Sportpesa, Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Uhusiano Sabrina Msuya Kushiriki, mteja atatakiwa kupiga *150*60# kisha kutuma pesa kwenye akaunti ya SportPesa namba 150888 kisha kuweka kubashiri.
Meneja Uhusiano SportPesa Sabrina Msuya, akiongea na moja ya washindi wa AMSHA AMSHA USHINDE NA AIRTEL MONEY kwa kushirikiana na Sportpesa, Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Matukio Airtel Tanzania. Mteja atatakiwa kupiga *150*60# kisha kutuma pesa kwenye akaunti ya SportPesa namba 150888 kisha kuweka kubashiri.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad