HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 9 July 2018

Wafanyabiashara wafurahishwa na zoezi la usajili kwenye Mfumo wa TANePS

Baadhi ya wafanyabiashara wameonesha kufurahishwa na namna mfumo mpya wa ununuzi kwa njia ya mtandao – TANePS unavyofanya kazi. 

Wafanyabiashara hao waliotembelea banda la PPRA kwenye viwanja vya maonesho ya Sabasaba wameonesha pia kufurahishwa na namna zoezi la kujisajili kwenye mfumo huo linavyofanyika kwa urahisi, huku wakielezea mfumo huo huenda ukawa ufumbuzi wa changamoto nyingi zinazoikabili sekta ya uununuzi wa umma ikiwa ni pamoja na gharama kubwa na ucheleweshaji wa michakato ya ununuzi serikalini. 

“Nafurahi kwa sababu Serikali sasa imeamua kufanya mambo yake kidigitali zaidi na hili litatusaidia hasa sisi wafanyabiashara wapya ambao tunataka kufanya kazi na Serikali,” alisema bw. Athumani Ngoma, mmoja wa wafanyabiashara waliojisajili na mfumo wa TANePS. 

Naye Bi. Siganike Baruti, ambaye ni mtaalam wa mifumo ya habari wa PPRA alielezea kufurahishwa na namna ambavyo wadau wa ununuzi wa Umma, hasa wafanyabiashara, wanavyoupokea mfumo wa TANePS. “Hizi ni dalili njema kwani mafanikio ya mfumo huu yanategemea zaidi uungwaji mkono na wadau,” alisema Bi. Siganike. 

TANePS ni mfumo ulioandaliwa na PPRA ili kukidhi matakwa ya sheria ya ununuzi wa Umma, na unawezesha mchakato mzima wa ununuzi wa bidhaa, vifaa, huduma na kazi za ujenzi kufanyika kwa njia ya mtandao (kielektroniki). 
Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA CPA Pius Maneno akipata huduma kutoka kwa watumishi wa PPRA
Mtaalam wa Mifumo ya Habari wa PPRA akiendelea na zoezi la usajili wa wafanyabiashara kwenye mfumo mpya wa ununuzi kwa njia ya mtandao (TANePS)
Mtaalam wa Mifumo ya Habari wa PPRA Bi. Siganike Baruti akitoa maelekezo ya namna ya kujisajili kwenye Mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya mtandao (TANePS) kwa mmoja wa wafayabiashara waliowatembelea
Mwanasheria wa PPRA Bi. Maria Mng'ong'o akimuhudumia Bi. Lilian Rugatika kutoka Chuo cha Uhasibu - Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad