HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 9 July 2018

UN yatunuku ubunifu katika maendeleo endelevu

 LATIFA Mohammed Ngea kutoka Zanzibar ameibuka kidedea katika tuzo za Umoja wa Mataifa za ubunifu na kupata hundi ya shilingi milioni 3. 
Latifa ni miongoni mwa vijana watatu waliokuwa wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa Mataifa, kwenye viwanja vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalifanyika. 
Latifa alipata tuzo hiyo kwa kubuni mfumo unaojiendesha wenyewe wa umwagiliaji katika kilimo. 
Mfumo huo unaojiendesha wa umwagiliaji maji unaweza kutumia king’amuzi ili kubaini wapi pana unyevu na wapi pakavu ili maji yaweze kupelekwa. 
Tangu kuanza kwa maonesho hayo takribani wiki sasa, wageni mbalimbali wamepata nafasi ya kuona ubunifu wa vijana hao katika roboti, sanaa na kilimo.
Aidha walionesha ubunifu wao unavyofanyakazi sanjari na kauli mbiu ya sabasaba mwaka huu inayosema “Kukuza biashara kwa maendeleo ya viwanda”. 
Baada ya wananchi kuwasikiliza wabunifu wote watatu, wageni walipata fursa ya kupiga kura nani waliamini alionyesha ubunifu bora zaidi, ndipo Latifa alipoibuka mshindi. 
Mbunifu mwingine alikuwa ni Gracious Fanuel anayetoka mkoani Kilimanjaro alipata ushindi wa pili. Huyu yeye alitengeneza roboti kwa kutumia vifaa vinavyopatikana majumbani. 
Roboti aliyotengeneza ni mfano wa Mkono ambao unaweza kuendeshwa kwa simu ya mkononi na anatarajia kukuza ubunifu wake ili ufikie hatua ya kuwa na mkanda wa uzalishaji bidhaa na pia kusaidia watu wenye ulemavu.
Mbunifu mwingine ni Amos Mtambala, kutoka Dar es Salaam, ambaye anatumia kipaji chake cha sanaa kwa shughuli za kijasiriamali yeye alishika nafasi ya tatu. Amos alipata mafunzo kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO) na tangu hapo amekuwa akipanua mtandao wake na kuwachukua zaidi ya vijana 100 ambao hutengeneza kazi za sanaa na kuuza nchini na pia kimataifa. 
Zaidi ya watu 500 katika Viwanja vya Sabasaba na kupitia mitandao ya kijamii walipiga kura kwa kijana yule wanayeamini aliandaa ubunifu bora zaidi. 
Mshindi wa kwanza alipata shilingi milioni 3 huku mshindi wa pili akipata shilingi milioni 2 na wa tatu shilingi milioni 1. 
Wabunifu hao watatu walikuwa miongoni mwa vijana 100 kutoka nchi nzima walioshinda ili kuonyesha ubunifu wao katika banda la UN. Hawa walichaguliwa kwa umakini ili kuendana na ujumbe wa mwaka huu wa Sabasaba, ambao ni Kukuza Biashara kwa Maendeleo ya Viwanda. 
Akizungumza katika banda la maonyesho la Umoja wa Mataifa wakati wa kutangaza washindi, Mtaalamu wa Mawasiliano wa UN, Bi. Hoyce Temu, aliwapongeza vijana ambao kwa kuwa na ndoto ya serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha kwamba azma ya maendeleo ya viwanda inatimia. 
Banda la maonyesho la UN ambalo Jumatano lilitangazwa kushika nafasi ya kwanza katika eneo la Utoaji Taarifa, Machapisho, Habari na Mawasiliano kwa jamii ni moja ya mabanda yaliyokuwa na pilika nyingi. 
Kupatikana kwa Tuzo hiyo iliyokabidhiwa na Waziri Mkuu, Mh. Kassim Majaliwa, wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam kumetokana na mkazo wa banda hilo mwaka huu la kutoa taarifa za matokeo na ushaiishaji wa UN katika Ubunifu kwa ajili ya Maendeleo Endelevu.
Umoja wa Mataifa Tanzania umeshinda nafasi ya kwanza katika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam mara kadhaa tangu UN ilipoanza kushiriki, kwani imeshiriki mara 8 mfululizo. Umoja wa Mataifa una nia ya kuendelea kushiriki ili kuwafikia watu wengi zaidi walio nje ya mfumo rasmi katika muktadha wa Sabasaba na Nanenane.
Kikosi Kazi cha Mawasiliano cha Umoja wa Mataifa (UNCG), ambacho ni kundi linalojumuisha maofisa wote wa Mawasiliano kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayofanya kazi nchini Tanzania, lina wajibu wa kubuni na kusimamia maandalizi ya banda la maonyesho.
 Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Bi. Hoyce Temu (kushoto) akimkabidhi Latifa Mohammed Ngea kutoka Zanzibar (kulia) mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni tatu mara baada ya kuibuka mshindi wa kwanza wa tuzo za Umoja wa Mataifa za ubunifu akiwa miongoni mwa vijana watatu waliokuwa wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa Mataifa, kwenye viwanja vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalifanyika. 
 Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Bi. Hoyce Temu (kushoto) akimkabidhi Gracious Fanuel kutoka Kilimanjaro (kulia) mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni mbili mara baada ya kuibuka mshindi wa pili wa tuzo za Umoja wa Mataifa za ubunifu akiwa miongoni mwa vijana watatu waliokuwa wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa Mataifa, kwenye viwanja vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalifanyika. 
 Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Bi. Hoyce Temu (kushoto) akimkabidhi Amos Mtambala kutoka Dar es Salaam (kulia) mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni moja mara baada ya kuibuka mshindi wa tatu wa tuzo za Umoja wa Mataifa za ubunifu akiwa miongoni mwa vijana watatu waliokuwa wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa Mataifa, kwenye viwanja vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalifanyika. 
 Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Bi. Hoyce Temu akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tuzo za Umoja wa Mataifa za ubunifu kwa vijana watatu waliokuwa wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa Mataifa, kwenye viwanja vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalifanyika. 
 Mshindi wa kwanza Latifa Mohammed Ngea kutoka Zanzibar aliyebuni mfumo unaojiendesha wenyewe wa umwagiliaji katika kilimo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea tuzo ya Umoja wa Mataifa ya ubunifu akiwa miongoni mwa vijana watatu waliokuwa wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa Mataifa, kwenye viwanja vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalifanyika. 
 Mshindi wa pili Gracious Fanuel kutoka Kilimanjaro aliyebuni roboti kwa kutumia vifaa vinavyopatikana majumbani akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea tuzo ya Umoja wa Mataifa ya ubunifu akiwa miongoni mwa vijana watatu waliokuwa wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa Mataifa, kwenye viwanja vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalifanyika. 
 Mshindi wa tatu Amos Mtambala kutoka Dar es Salaam, ambaye anatumia kipaji chake cha sanaa kwa shughuli za kijasiriamali akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea tuzo ya Umoja wa Mataifa ya ubunifu akiwa miongoni mwa vijana watatu waliokuwa wakionesha ubunifu wao katika banda la Umoja wa Mataifa, kwenye viwanja vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalifanyika. 
 Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Bi. Hoyce Temu akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa kwanza Latifa Mohammed Ngea kutoka Zanzibar (katikati), mshindi wa pili Gracious Fanuel kutoka Kilimanjaro (kushoto) pamoja na mshindi wa tatu Amos Mtambala kutoka Dar es Salaam (kulia) huku wakiwa wameshikilia hundi zao.
Mshindi wa kwanza Latifa Mohammed Ngea kutoka Zanzibar (katikati), mshindi wa pili Gracious Fanuel kutoka Kilimanjaro (kushoto) pamoja na mshindi wa tatu Amos Mtambala kutoka Dar es Salaam (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na mfano wa hundi waliozokabidhiwa na Umoja wa Mataifa wakati katika banda la Umoja wa Mataifa, kwenye viwanja vya sabasaba, ambako Maonyesho ya Biashara ya 42 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yalifanyika. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad