HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, July 5, 2018

UKAGUZI WA MAGARI KILIMANJARO WABAINI ,MADEREVA KUTUMIA LESENI ZA NDUGU ZAO

Kamanda wa Polisi akimuuliza mmoja wa madereva waliokamatwa, matumizi ya silaha ya Kisu kilichokutwa katika gari lake.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii KAnda ya Kaskazini. 


UKAGUZI wa Magari ya Abiria pamoja na Leseni unaofanywa na Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro umebaini udanganyifu mkubwa unaofanywa na baadhi ya Madereva wa Magari ya abiria ukiwemo kuendesha bila Leseni ,Umri wa kuendesha gari kupitiliza , wengine wakitumia Leseni za Ndugu zao.

Katika kituo Kikuu cha Mabasi ya abiria yaendayo mikoani na yale yanayofanya safari zake ndani ya mkoa wa Kilimanjaro,Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Hamisi Issah akiwa ameongozana na Mkuu Operesheni kikosi cha usalama Barabarani ,Peter Mizambwa na maofisa wengine wa Polisi wamefanya ukaguzi.

Katika ukaguzi huo magari zaidi ya 800 yamekaguliwa na yaliyobainika kuwa mabovu yalizuiliwa kuendelea na safari huku baadhi ya Madereva wakikutwa na silaha katika magari yao vikiwemo Visu,kamanda Issah akatoa onyo kwa madereva kutembea na silaha pamoja na kujaza abiria hali inayochangia abiria kukaa katika mikao isiyo rafiki .

Mkuu wa operesheni wa kikosi cha usalama barabarani ,Mkaguzi wa Polisi Peter Mizambwa akazungumzia Operesheni Nyakua iliyoanza kwa lengo la kupunguza ajali huku baadhi ya Madereva na wananchi wakipongeza utaratibu huo.

 Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, ACP Hamis Issah akitembelea kikuu cha Mabasi mjinib Moshi kwa ajili ya ukaguzi wa Magari ya Abiria. 
 Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,ACP.Hamis Issah akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Operesheni wa kikosi cha Usalama Barabarani,Mkaguzi ,Peter Mizambwa wakati wa ukaguzi huo uliofanyika katika kituo kikuu cha Mabasi mjini Moshi. 

 Mkuu wa Operesheni wa Kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Kilimanjaro,Inp Peter Mizambwa akimuonesha kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,ACP,Hamis Issah moja ya karatasi ambazo zinatumiwa na madereva kama Leseni.
 Mkuu wa Operesheni wa Kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Kilimanjaro,Inp Peter Mizambwa akimuonesha kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,ACP,Hamis Issah alama za leseni ambayo ni halisi . 
 Kamanda Issah akitoa maelekezo kwa askari wake. 
 Mmoja wa Madereva waliokaguliwa akionesha vipande vya karatasi ambavyo alidai kuwa ni leseni.
Mkaguzi wa Magari akikagua moja ya mabasi yaliyokuwa yafanye safari ya kuelekea Dar es Salaam
Mmoja wa Madereva akipelekwa kituo cha Polisi mara baada ay kubainika kutumia leseni ya ndugu yake kuendesha gari.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad