HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 5 July 2018

Tume ya Uchaguzi yamuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (kulia) akimkabidhi ua aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani ikiwa ni ishara ya kumuaga na kumtakia kila la kheri katika kutekeleza majukumu ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (katikati) akizungumza kwenye kikao cha kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani  ambaye kwa sasa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.Kushoto ni Mkurugenzi mpya wa Uchaguzi Dkt. Athumani Kihamia.
 Aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani  ambaye kwa sasa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akizungumza kwenye kikao cha Tume cha kumuaga.Katikati  ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage na  Mkurugenzi mpya wa Uchaguzi Dkt. Athumani Kihamia.
Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura Giveness Aswile akitoa neno la kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani  kwa niaba ya wakuu wa Idara  za Tume wenzake.Kilia ni Mkuu wa Idara ya Uendeshaji Uchaguzi Irene Kadushi.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage (kulia) akimpa mkono wa kumuaga aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhani ambaye kwa sasa ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.Kushoto ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt. Athumani Kihamia.
Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt. Athumani Kihamia akimpa mkono wa kumuaga Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Bw. Kailima Ramadhani .Katikati ni Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (R) Semistocles Kaijage. Picha na Hussein Makame-NEC

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad