HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, July 6, 2018

TFDA iwe chachu ya Uchumi wa Viwanda nchini.



Na  WAMJW, Dar as Salaam
Mamlaka ya chakula na dawa TFDA imetakiwa kuwa chachu ya uchumi wa viwanda hususani katika kuzalisha dawa hapa nchini ili kupata matokeo chanya katika hatua ya kuinua uchumi wa viwanda.

Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati wa kukabidhi vyeti vya ithibaki kwa kiwango cha kimataifa ISO 17025 kwa maabara ya chakula na maikrobailojia za TFDA.

"TFDA isiwe kikwazo kwa wawekezaji nchini hususan Viwanda vya kuzalisha dawa ili kuunga mkono juhudi za Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli ya kuelekea uchumi wa viwanda"

Aidha,Waziri Ummy amesema TFDA wanawajibu wa kuwawezesha wafanyabiashara kutoa bidhaa zao wanazozileta nchini mapema zaidi Mara wanapokuwa wamejiridhisha na ubora unaokidhi afya za watanzania na kuwapa vibali mapema.Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA )Agnes's kijo amesema wanawajibu wa kuimarisha afya za watanzania na kuimarisha maabara zao kwa viwango vinavyokubalika kitaifa.

Kijo amesema vyeti hivyo vya kimataifa ni ishara kubwa inayoonyesha Kuwa TFDA inafanya kazi katika kudhibiti ubora wa bidhaa hususan vyakula na dawa ili kujenga afya za wananchi.TFDA imepokea vyeti vya uthibiti kwa kiwango cha kimataifa kwa maabara ya chakula na daea ambapo wamefanya vizuri katika upimaji wa vyakula na dawa vinavyoingia na kutoka nchini.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA na baadhi ya wadau wa afya hawapo pichani wakati wa upokeaji wa vyeti vya Ithibati kwa kiwango cha kimataifa iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA Bi. Agness Kijo akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka hiyo na baadhi ya wadau wa afya hawapo pichani wakati wa upokeaji wa vyeti vya Ithibati kwa kiwango cha kimataifa iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wa kushoto akikata utepe kuashiria kupokea rasmi vyeti vya Ithibati kwa kiwango cha kimataifa walivyopewa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA katika hafla ya kupokea vyeti hivyo leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa Maabara wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA wakati wa upokeaji wa vyeti vya Ithibati kwa kiwango cha kimataifa iliyofanyika leo jijini Dar es salaam, wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa TFDA Bi. Agness Kijo.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Sehemu ya tendaji wa Mamlaka ya chakula na dawa

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad