



Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
JESHI la
Polisi mkoani Kilimanjaro limekagua Leseni za Madereva 2182 ,madereva 13
wakibainika kutumia Leseni za madaraja yasiyoruhusu kuendesha Magari ya Abiria
huku Madereva watatu wakishikiliwa kwa kosa la kuendesha gari bila ya kuwa
leseni.
Katika
ukaguzi huo uliofanyika kwa muda wa wiki moja katika mkoa wa Kilimanjaro ,Jeshi
la Polisi pi limebaini uwepo wa madereva waliovuka umri wa kuendesha gari kwa
mujibu wa sheria ambao ni miaka 60 huku likiwataka kuacha mara moja kuendelea
na kazi hiyo.
Kutokana na
mapungufu mbalimbali yaliyobainika kwa Madereva wa Magari ya Abiria ,Jeshi la
Polisimkoa wa Kilimanjaro likatangaza kuanza mafunzo kwa Madereva wa magari ya
Abiria yanayofanya safari zake ndani na nje ya mkoa wa Kilimanjaro ikiwa ni
pamoja na maelekezo ya alama mpya za barabarani.
Akizungumza
kwa niaba ya Madereva,Dereva mzoefu wa magari makubwa ,Apolonary Malya
amepongeza utaratibu huo wa jeshi la Polisi kutoa mafunzo ikiwa ni sehemu ya
kuwakumbusha madereva baadhi ya sheria ya usalama barabarani.
Mafunzo kwa
madereva hao yameanza kutolewa katika ukumbi mdogo uliopo ofisi za kikosi cha
usalama barabarani mkoa wa Kilimanjaro chini ya Mkuu wa kikosi hicho Mrakibu
msaidizi wa Polisi Zauda Mohamed na maofisa wengine wa Polisi .
No comments:
Post a Comment