HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 11, 2018

Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi awaondoa hofu wafugaji wa samaki

NAIBU waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amewaondoa hofu wafugaji wa samaki kuhusu suala la upimaji wa samaki hao kwa rula huku akidai sheria hiyo inalenga zaidi samaki Wanaovuliwa Ziwa Victoria pekee na si kwingineko.

 Amesema kuna hofu ambayo inaweza kujengeka katika uvuvi wa samaki nakudai kwamba kwa watu ambao wanafuga samaki wao kitu cha kuzingatia kabla hawajaaza kuwavua kwa ajili ya kuwaingiza sokoni ni vema kuwashirikisha watalaamu ambao wanakuwa nao katika maeneo yao.

 Ulega ameyasema hayo jana kwenye viwanja vya maonesho yanayoendelea katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es salaam ambapo alitembelea Banda la wizara ya Uvuvi na mifugo na baadae kuendelea na ziara yake katika mabanda mengine.

 Amesema kuwa kulikuwa na mjadala mkubwa kuhusu rula huku wengine wakimuuliza inakuaje kwa watu wanaofuga ambapo alisema hakuna shaka yeyote badala yake waendelee kufuga kwa wingi ili kuchochea ukuwaji wa uchumi wa viwanda nakwamba wakati wa kuwavuna nivema wakashirikisha wataalamu.

 Waziri Ulega pia amewataka watanzania hususani wafugaji na wavuvi kutembelea katika banda la wizara yake ili kupata mafunzo juu ya kufuga samaki lakini pia mifugo mbalimbali.

 Akizungumzia ufugaji wa mifugo alisema niwakati stahiki sasa wafugaji kujenga nidhamu ya kuvuna manyasi ili wakati wa kiangazi wasipate shida ya majani ya kulisha.

 "Ndugu zangu waandishi katika kipindi cha mwaka huu mvua imenyesha kwa wingi ilikuwa ni wakati sahihi kwa ndugu Zangu wafugaji kuvuna manyasi na kuweka katika marobota ambapo ng'ombe wawili wanauwezo wa kula robota moja na wakashiba. "alisema Ulega

 Ameongeza kwa kutoa rai kwa wafugaji kuhakikisha wanatumia mvua zinazonyesha kuweza kuvuna marobota ya manyasi ili mwisho wasiku hususani nyakati za kiangazi waje kulisha mifugo yap.

 Pia amesema mbali na ufugaji wa samaki lakini pia wanafundisha mambo mbalimbali hivyo niwananchi kwenda katika banda lao lililopo sabasaba na hata baada ya sabasaba kufika kwenye ofisi zao wataalamu watatoa mafunzo yanayo husu ufugaji, na uvuvi.


Akizungumza mara baada ya kutembelewa  na Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega katika banda lake la woiso ambalo linabidhaa halisi za ngozi   Meneja Masoko Teya Herman alisema changamoto kubwa wanayokutana nayo ni uharibifu wa ngozi inayotumika kutengeneza bidhaa hizo 

Amesema kuwa mara nyingi wanakuta ngozi imeharibika na hiyo nikutokana na ng'ombe hizo kupigwa chapa ambazo zinaharibu ngozi hivyo ameomba serikali kuangalia upya namna ya maandalizi ya ngozi hizo. 

Pia Teya amesema licha ya ngozi kuwa inaharibika lakini wao kama Woiso wanatengeza bidhaa bora na za kisasa na imara kuliko mahala pengine popote. 

Amesema Kwa sasa wapo sabasaba na baada ya hapo wanapatikana barabara ya kwenda salasala na kimsingi wameamua kuitikia wito wa Rais Magufuli kutengeza viwanda vidogovigo.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akiangalia samaki katika banda la Wizara hiyo.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akipewa maelezo ya ufugaji wa bata wakati alipotembelea banda la JKT katika maonesho ya 42 ya biashara Kimataifa katika viwanja vya Mwalim Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akipewa maelezo ya ufugaji wa kuku wakati alipotembelea banda la JKT katika maonesho ya 42 ya biashara Kimataifa katika viwanja vya Mwalim Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akipata maelezo kutoka kwa Meneja Masoko wa Kampuni ya Woiso Original Products Teya Herman kuhusiana na bidhaa ngozi zinazolishwa kampuni Woiso wakati alipotembelea banda Woiso katika maonesho ya Sabasaba.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya Woiso Original Products wakati alipotembelea banda Woiso katika maonesho ya Sabasaba.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad