HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 11 July 2018

KAMANDA MATEI AIBUKIA KITUO CHA MABASI MBEYA

Na Emanuel Madafa, Mbeya
Zikiwa zimepita siku tisa tangu, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Saimon Siro, kufanya mabadiliko ya Makamanda wa Polisi, Kamanda wa Mkoa wa Mbeya, Kamishina Msaidizi Mwandamizi(SACP) Ulrich Matei, ameanza kazi kwa kukagua mabasi ya abiria ya Mikoani Mbeya na kuwapima madereva ulevi.

Katika zoezi hilo, basi la Kampuni ya Premier linalofanya safari zake mkoani Mbeya na Mwanza, lilibainika kuwa na kasoro kwenye mfumo wa usukani hivyo kuzuiwa kusafirisha abiria hadi pale tatizo hilo litakapo tatuliwa.

Akizungumza katika kituo cha mabasi Matei amesema, madereva wa magari yote yakiwemo yanayosafirisha abiria wanatakiwa kuzingatia sheria za usalama barabarani huku wamiliki wa mabasi wakitakiwa kuhakikisha wanafanya matengenezo ya vyombo hivyo kabla ya kuanza safari zake.

Amesema  lazima watu watii sheria bila shuruti, hivyo kama unafahamu chombo chako kibovu basi kiwekwe pembeni ili kuepuka kukutana na mkono wa sheria .

Aidha, akizungumzia mkakati wa jeshi hilo katika kupunguza vitendo vya uhalifu, Kamanda aliwataka wananchi kuendelea kutoa taharifa kwani hizo ndizo zitakazo saidia kukomesha tabia za wahalifu.

Amesema pia wataendelea kutoa elimu  kwa jamii ili kuepuka vtendo vya kihalifu ambavyo vinatokea kutokana jamii kukosa elimu katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishina Msaidizi Mwandamizi (SACP) Ulrich Matei akimpima mmoja wa madarerva wa mabasi ya abiria katika kituo kikuu cha mabasi Mbeya leo Julai 11, 2018.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishina Msaidizi Mwandamizi(SACP) Ulrich Matei akiongoza askari wa ukaguzi wa magari na leseni katika kituo kikuu  cha Mabasi Mbeya.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad