HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 2, 2018

Mratibu wa UN azuru maonesho ya sabasaba

MRATIBU Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro Rodriguez ametembelea maonesho ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam. Akiwa katika maonesho hayo, maarufu kama ya Sabasaba alikutana na Mkurugenzi Mkuu wa Tan Trade, Bw. Edwin Rutageruka.

Katika mazungumzo hayo walijadiliana masuala mbalimbali zikiwamo changamoto na fursa za kibiashara na viwanda zinazojitokeza kwa sababu ya kuwapo kwa maonesho hayo kwa Tanzania na Afrika Mashariki. Baada ya mazungumzo hayo, Mratibu huo alifanya ziara katika mabanda kadhaa akianzia na banda la Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini.

Mwaka huu banda la Umoja wa Mataifa lina wabunifui vijana watatu ikiwa ni sehemu ya shughuli ya Umoja huo ya kuibua na kukuza ubunifu kwa maendeleo endelevu. Ukitembelea banda hilo utakutana na Gracious Fanuel ambaye alivumbua mkono wa roboti ambao unaweza kuendeshwa na simu ya mkononi.

Ni matumaini yake kwamba uvumbuzi huo unaweza kuboreshwa zaidi na kutumika katika viwanda mbalimbali. Mbunifu mwingine ni Latifa Mohammad Ngea kutoka Zanzibar ambaye amevumbua mfumo wa umwagiliaji ambao ni automatiki na inatumia ‘sensa’ kutambua kama ardhi ina unyevunyevu na kupeleka maji katika maeneo makavu.

Pia katika banda hilo la Umoja wa Mataifa utakutana na Amos Mtambala ambaye anatumia uwezo wake wa kiusanii kufanya ujasiriamali. Amos ambaye amefunzwa na kupewa ufadhili na Shirika la Kazi Duniani (ILO) ametanua shughuli zake na kuingiza vijana zaidi ya 100.

Pamoja na kuwapo kwa wabunifu hao, Umoja wa Mataifa unaendesha shindano la wavumbuzi vijana. Watu wanaofika katika banda la Umoja wa Mataifa wataweza kupata nafasi ya kuwapigia kura wavumbuzi hao ili kujua nani ni bora zaidi.

Imeelezwa na Umoja wa Mataifa kwamba kura hizo zitawezesha kumpata mbunifu bora atakayepewa tuzo na zawadi! Unaweza pia kuingia katika twita za Umoja wa mataifa @UnitedNationsTZ kuona video za wabunifu hao na kupiga kura kupitia twita.

Mratibu huyo wa Umoja wa Mataifa pia alitembelea mabanda kadhaa likiwamo banda la SIDO. Akiwa katika banda hilo alijionea mashine na bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa na wajasiriamali waliofadhiliwa na SIDO.

Kwa miongo kadhaa UN imekuwa ikifanyakazi kwa ushirikiano na SIDO na imekuwa ikisaidia vijana kupata mashine kwa ajili ya shughuli mbalimbali zikiwamo za kusindika zao la muhogo.
 Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Bw. Edwin Rutageruka alipotembelea viwanja vya Sabasaba vilivyopo Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam .
 Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akiwa kwenye mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Bw. Edwin Rutageruka katika chumba maalum cha wageni mashuhuri alipotembelea maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
 Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) akizungumza jambo na Mkuu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu (wa pili kulia) pamoja na Afisa Uhusiano wa Shirika la Kazi nchini (ILO), Magnus Minja wakati wakielekea kwenye banda la Umoja wa Mataifa katika maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
 Afisa Uhusiano wa Shirika la Kazi nchini (ILO), Magnus Minja (kushoto aliyenyoosha kidole) akitoa maelezo kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez kuhusu uvumbuzi uliofanywa na kijana Gracious Fanuel wa roboti anayeweza kufanyakazi kwa kupitia mifumo ya simu, roboti huyo anaweza kutumika katika shughuli mbalimbali za viwandani wakati alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa katika maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
 Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez akiwasilikiliza vijana wabunifu Gracious Fanuel na Latifa Mohammad Ngea kutoka Zanzibar wakati alipotembelea Banda la Umoja wa Mataifa katika maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
 Mbunifu Lafita Mohammad Ngea  kutoka Zanzibar aliyebuni mifumo ya automatiki yenye sensa ya umwagiliaji ambayo hutambua eneo lenye unyevu na kavu na kupelekea maji kwenye maeneo makavu katika Banda la Umoja wa Mataifa katika maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
 Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na Ofisa wa Mawasiliano kwa Umma wa TanTrade, Daniel Diha wakati alipotembelea Banda la Umoja wa Mataifa katika maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
 Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez akipata maelezo kutoka mwanamke mjasiariamali kutoka Zanzibar alipotembelea banda la SIDO katika maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
 Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez akiwa nje ya banda la kituo cha redio cha Efm lililopokatika maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
 Mbunifu Lafita Mohammad Ngea  kutoka Zanzibar akitoa maelezo namna ya ubunifu wake unavyoweza kufanya kazi kwa mmoja wa mwananchi aliyetembelea Banda la Umoja wa Mataifa katika maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Kijana mbunifu Gracious Fanuel mvumbuzi wa roboti anayeweza kufanyakazi kwa kupitia mifumo ya simu, roboti huyo anaweza kutumika katika shughuli mbalimbali za viwandani akiwa katika banda la Umoja wa Mataifa katika maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad