HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 7 July 2018

MMILIKI WA KIWANDA ASHIKILIWA NA JESHI LA POLUSI MKOA WA PWANI KWA TUHUMA ZA KUHUSIKA NA UCHOMAJI WA KIWANDA HICHO

 Na Linda  Shebby, Pwani


JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia mmiliki wa kiwanda cha kuchapisha nyaraka  mbalimbali kinachofahamika kwa jina la Yukos Enterprises  kilichopo katika eneo la Tondoroni Kata ya Kisarawe Mkoa wa Pwani  aliyetajwa kwa jina la Magora Magira Masegese kwa tuhuma za kukihujumu kiwanda hicho kwa kukichoma moto katika  majengo makubwa mawili  yenye mitambo  mbalimbali  yaliyopo katika kiwandani hapo.

Akizungumza leo katika mkutano na waandishi wa  habari  Kaimu Kamanda  wa Polisi  Mkoa wa Pwani SSP   Blasius Chatanda  amesema kuwa Jeshi la Polisi pia  linamshikilia  Meneja  wa Kiwanda hicho  Elia Elson  pamoja na  walinzi wawili  ambao ni Sai Kwilasa na Razi Kadilio kwa mahojiano zaidi na kuwa thamani ya mali  iliyoungua bado haijafahamika hadi hivi sasa.

"Baada  ya taarifa kutufikia tuliwasiliana na wenzetu  wa zimamoto  na kuweza  kufanikiwa  kufika  kwa wakati  na kuuzima moto  huo kabla  haujaenea  kwenye majengo mengine yaliyopo kwenye kiwanda hicho" alisema Kaimu Kamanda  wa Polisi Mkoa wa Pwani SSP Chatanda.

Aidha Kalimu Kamand alisema kuwa  baada ya jeshi hilo kufanya ukaguzi  katika moja ya jengo  ambalo moto uliwahi kuzimwa , walikuta majaba matano  yaliyokuwa kwenye  kona  ya jengo hilo ndani  yake  kukiwa na  mafuta  aina ya petroli pamoja na karatasi  rola  lililokuwa limetandikwa  kwenye korido za jengo hilo  ambalo ndani  yake kulikuwa  na nyaraka  mbalimbali ambazo  zilikuwa  zimemwagiwa  mafuta  ya petroli lakini hazikuweza  kuungua.

Aidha  Mrakibu  Msaidizi   huyo wa Jeshi  la Zimamoto Mkoa wa Pwani Happines Shirima amesema  changamoto waliyokumbana nayo walipofika ni kutoka kwa mmiliki wa kiwanda hicho aliposhindwa kuwafungulia lango kuu kwa madai kuwa mtoto wake ndiye anayejua zilipofunguo gali iliyochangia wafikie uamuzi wa kuvunja mlango ili kuweza kuwaokoa  baadhi ya wafanyakazi ambao walikuwemo ndani ya kiwanda gicho wakati kikiwaka moto.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad