HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, July 1, 2018

BREAKING NEWS: RAIS DKT. MAGUFULI AFANYA MABADILIKO MADOGO KATIKA BARAZA LA MAWAZIRI, KANGI LUGOLA ACHUKUA NAFASI YA MWIGULU NCHEMBA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo amefanya mabadiliko madogo katika baraza lake la Mawaziri, ambapo amemteua aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Kangi Alphaxard Lugola kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, kuchukua nafasi ya Mwigulu Lameck Nchemba.

Rais Magufuli amefanya mabadiliko hayo alasiri hii kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu, Balozi John Willium Kijazi.

Kwa mujibu wa Balozi Kijazi, nafasi ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), inachukuliwa na Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Musa Ramadhani Sima. 

Aidha Rais ameongeza nafasi ya uteuzi wa Naibu Waziri katika Wizara ya kilimo kutokana na umuhumu wa Wizara hiyo ambapo, Mbunge wa Morogoro Kusini, Omary Mgumba ameteuliwa kushika nafasi hiyo.

Katika mabadiliko hayo madogo, Rais Magufuli amefanya Uhamisho wa Waziri Prof. Makame Mbarawa kutokea Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na sasa anaenda kuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, huku aliyekuwa kwenye Wizara hiyo, Mhandisi Isack Kamwelwe anaenda kuwa Waziri wa Uchukuzi.

Balozi Kijazi amesema tarehe ya kuapishwa kwa viongozi hao itatajwa hapo baadaye.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi akitangaza majina ya Viongozi mbalimbali walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad