HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 3, 2018

BENKI YA TIB CORPORATE YAWATAKA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LAO NDANI YA VIWANJA VYA SABASABA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Benki ya TIB Corporate imewataka wananchii kujitokeza kwenye banda lao lililopo ndani ya maonesho ya 42 ya Sabasaba na kuweza kufungua akaunti za benki hiyo ili waweze kujivunia faida kibao kwa kuweka hela zao Kwenye benki ya  TIB.

Akizungumza na Michuzi Blog Mkurugenzi wa Huduma za Matawi na Masoko wa Benki ya TIB Corporate Theresia Msoka amesema kuwa Benki ya TIB Corporate imezindua aina tofauti nne za akaunti ambazo zitamuwezesha mteja wa benki hiyo kufungua akaunti na kuhifadhi fedha zake kwa uhakika zaidi.

Amesema kuwa benki yao ni ya kibiashara ila inawahudumia wananchi wote wakiwemo watu binafsi, taasisi au makampuni pamoja na kuwawezesha kupata mikopo ya haraka sana kwa ajili ya kufungua au kuendeleza biashara zao ikiwemo viwanda.

Bi Theresia amesema kwa mwaka huu wamekuja na kauli mbili ya "JIPANGE NA TIB CORPORATE BANK" ambao wamewaletea  akaunti nne tofauti zitakazomuwezesha mwananchi kuhifadhi fedha zake na kujipatia riba kubwa zaidi kadri anavyoweka hela ukiweka fedha kwenye akaunti ya Flex inayopatikana ndani ya benki yao.

Meneja wa Fedha wa Benki ya TIB Corporate June Magingi ameelezea kuwa katika moja ya akaunti za Jipange ni akaunti ya Toto Bank ya chini ya umri wa miaka 18 unayoweza kumuwekea fedha kwa ajili ya akiba yake baadae itakayomsaidia ikiwemo kulipia masomo yake.

Meneja Mahusiano wa Benki ya TIB Corporate Majaba Magana ameelezea kuwa akaunti ya Jamii ni akaunti ya hundi na haina gharama yoyote inayofaa kutumiwa na hususani mashirika ya umma, taasisi binafsi na kidini, Mifuko ya hifadhi kama vile Saccos, Vicoba na hata NGO's.

Ofisa Huduma kwa Wateja  Benki ya TIB Corporate Janeth Burton amewataka watanzania kufungua akaunti ya Fix akaunti itakayomuwezesha mteja kupata riba kubwa pindi pale anapokuwa anaweka fedha zake kila mara.
 Mkurugenzi wa Huduma za Matawi na Masoko wa Benki ya TIB Corporate Theresia Soka akielezea huduma wanazozitoa ndani ya banda lao pamoja na kuwafungulia wananchi akaunti hapo hapo kwenye maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Kibiashara yanayoendelea Katika Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar Es Salaam.
 Meneja wa Fedha wa Benki ya TIB Coorporate June Magingi na  Ofisa huduma kwa wateja  Janeth Burton (kulia) Wakimpatia maelekezo mteja aliyefika katika banda lao la maonyesho lililopo ndani ya Viwanja vya Sabasaba katika maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Kibiashara yanayofanyika Jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Masoko wa Kampuni ya Masasi Food Production Secky Nyewa akielezea namna Benki ya TIB ilivyoweza kuwapatia mkopo na kuwezesha kufungua kwa kiwanda hicho kinachotengeneza bidhaa za chakula ndani ya  maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Kibiashara yanayofanyika ndani ya Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi akielezea jambo mbele ya Mkurugenzi wa Huduma za Matawi na Masoko Theresia Soka  wa Benki ya TIB Coorporate (kushoto) na Mkuu wa Utafiti wa Maendeleo ya Benki TIB Coorporate Dr Hildebrand Shayo alipotembelea banda ya benki hiyo ndani ya maonyesho ya 42 ya kimataifa ya biashara yanayoendelea ndani ya Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Matawi na Masoko Benki ya TIB Coorporate Theresia Soka akimuelezea jambo Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi alipotembelea banda la maonyesho la benki ya TIB lililopo ndani ya Viwanja vya Sabasaba  katika maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Kibiashara yanayofanyika Jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Utafiti wa Maendeleo ya Benki TIB Coorporate Dr Hildebrand Shayo akimuelezea jambo Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi alipotembelea banda la maonyesho la benki ya TIB lililopo ndani ya Viwanja vya Sabasaba  katika maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Kibiashara yanayofanyika Jijini Dar es Salaam.
  Wafanyakazi wa Benki ya TIB Coorporate wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya banda lao la Maonyesho kwenye Viwanja vya Sabasaba maonyesho ya 42 ya Kimataifa ya Kibiashara yanayofanyika Jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad