HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 24 July 2018

Airtel Money yaungana na serikali kurahisisha malipo kupitia mfumo wa GePG

Kampuni ya simu za mkononi inayoongoza kwa utoaji wa huduma bora za Smartphone Airtel Tanzania leo imetangaza kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango kupitia kitengo chake cha (Government Electronic Payment Gateway) katika kutoa suluhisho la malipo rahisi ya papo kwa hapo kupitia huduma ya Airtel Money. Kupitia mfumo huo, wateja wa Airtel Money sasa wataweza kulipia malipo ya huduma mbali mbali pamoja na tozo za serikali mahali popote kutoka kwenye simu zao kama vile ushuru, karo na malipo mengine yoyote.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati akitangaza ushirikiano huo, Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchunda alisema kuwa “idadi ya wateja wa Airtel Money imekuwa ikikua siku hadi siku na hivyo kupelekea kufanikisha moja kati ya malengo ya serikali yetu ya kuhakikisha kuwa inafanikisha upatikanaji wa huduma za kifedha kila mahali yaani mjini na vijijini. Pia mafanikio haya leo hii yanapelekea kuwezesha ukusanyaji wa kodi na mapato mbalimbali  ya serikali, Airtel tunawahimiza na kuwapa taarifa wateja wa Airtel Money kuwa tumeunganishwa sasa na GePG hivyo waendelee kutumia mfumo huu rahisi kulipia malipo mbalimbali kupia simu zao wakiwa popote”

Mfumo wa GePG ni kwa ajili ya kila mtanzania. “Nachukua fursa hii kuwaomba watanzania kutumia mfumo huu kwani ni salama, rahisi na nafuu”, alisema Nchunda huku akiongeza kuwa Airtel Tanzania imedhamiria kuendelea kuhudumia wateja kwa ubora wa hali ya juu kwa kuongeza idadi ya mawakala wa Airtel Money ambao kwa sasa wanafikia zaidi ya elfu 55.”Vile vile, tunaendelea kuongeza mawakala kupitia usambazaji wa vioski vya Airtel Money na kuongeza uekezaji katika maduka ya Airtel Money Branch ambayo sasa tayari yanatoa huduma kama wakala wa kawaida  na pia kama wakala mkubwa ambapo hadi sasa hivi tumeshafungua matawi (Airtel Money Branch) zaidi ya 300 yanayotoa wigo mkubwa zaidi wa mawakala nchini.

“Wateja wa Airtel Money wanachotakiwa kufanya ili  kulipa kodi au tozo mbalimbali za serikali piga *150*60# kuchangua namba 5 halafu 3 kisha weka kiwango cha malipo ikifuatiwa na namba ya kumbukumbu ya malipo kisha kulipia huduma yoyote papo kwa papo kama vile TRA, faini mbali mbali, LUKU, DAWASCO, pasi ya kusafiria, kodi ya majengo pamoja na malipo mengine”, alisema Nchunda.

Nchunda aliongeza kuwa Airtel itaendelea kuja na huduma na bidhaa nafuu zenye ubora wa hali ya juu huku akitolea mfano huduma mpya inayojulikana kama HAKATWI MTU HAPA – Tuma Pesa Bure ambayo inawawezesha wateja wa Airtel Money kutuma pesa bure bila makato yoyote kwa lengo ya kuwafikishia huduma za kifedha hapa nchini kwa kuwafikia Watanzania zaidi ya 80% ambao bado hawajafikiwa na huduma za kibenki.

Kwa upande wake Ofisa mwakilishi wa GePG kutoka wizara ya Fedha na Mipango Bw, Basil S. Baligumya aliipongeza kampuni ya Airtel Tanzania kwa kuweza kushirikiana na serikali kwenye mfumo wa (Government Electronic Payment Gateway) na kusema “Mfumo wa GePG ni moja ya mikakati ya serikali ya kufanya malipo kuwa rahisi na kuongeza uwazi. Nawaomba Watanzania watumie mfumo huu kwani ni maalum kwa watumiaji wote wanaotaka kufanya malipo  ya serikali kama ilivyo kwa watumiaji wa Airtel Money”.

Baligumya alisema kuwa “mfumo wa GePG unalenga kutoa huduma kwa wananchi kwa urahisi, kuongeza ufanisi katika malipo, kuongeza ukaribu kati ya wananchi na serikali na pia kwenye sekta ya biashara na kuleta mawasiliano karibu baina ya serikali na wananchi wake. Vile vile, mfumo utaongeza mapato serikalini kwani malipo yote yameunganishwa na hivyo mwananchi anaweza kufanya malipo wakiwa sehemu yoyote na kwa muda wowote” 
 Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchunda akiongea wakati wa  kutangaza kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango kupitia kitengo chake cha (Government Electronic Payment Gateway) katika kutoa suluhisho la malipo rahisi ya papo kwa hapo kupitia huduma ya Airtel Money. Kupitia mfumo huo, wateja wa Airtel Money sasa wataweza kulipia malipo ya huduma mbali mbali pamoja na tozo za serikali mahali popote kutoka kwenye simu zao kama vile ushuru, karo na malipo mengine yoyote. Kushoto ni Ofisa mwakilishi wa GePG kutoka wizara ya Fedha na Mipango Bw, Basil S. Baligumya na Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando.
Ofisa mwakilishi wa GePG kutoka wizara ya Fedha na Mipango Bw, Basil S. Baligumya akiongea wakati wa  kutangaza kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango kupitia kitengo chake cha (Government Electronic Payment Gateway) katika kutoa suluhisho la malipo rahisi ya papo kwa hapo kupitia huduma ya Airtel Money. Kupitia mfumo huo, wateja wa Airtel Money sasa wataweza kulipia malipo ya huduma mbali mbali pamoja na tozo za serikali mahali popote kutoka kwenye simu zao kama vile ushuru, karo na malipo mengine yoyote. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchunda na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Jackson Mmbando.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad