HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 29 June 2018

Young Killer aachia video ya ‘Hunijui’ akiwashirikisha Dully Sykes na Ben Pol

Rapper Young Killer Msodoki ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Hunijui’ aliomshirikisha mkongwe kwenye muziki wa Bongo Flava, Dully Sykes pamoja na mfalme wa R&B Tanzania, Ben Pol.

Kwa historia yake ya kutengeneza hits, haikuwa ngumu kuwapata wakubwa zake kuiwekea nakshi ngoma hii. Young Killer anasema alianza kumshirikisha Ben Pol kwanza na alipomtembelea Dully Sykes ili kumsikiliza wimbo,  muda huo huo staa huyo akaupenda na yeye kuridhia kuweka mchango wake.

“Nimempa nafasi Dully kwenye ngoma sababu ni legend na ni inspiration kwa watu wengi na niliowafuatilia tangu kitambo,” anasema Young Killer. “Na Ben Pol ni moja kati ya watu niliokuwa nawasikiliza wakipiga chorus za watu ambao walikuwa wamenitangulia, unasikia kabisa kuna kitu amekifanya na bila uwepo wake kisingekuwa. Nimewashirikisha sababu niliamini watafanya kitu kizuri ambacho wamekifanya,” ameongeza.

Young Killer anasema Hunijui ni ujumbe kwa watu wanaodhani kumjua vizuri wakati si kweli. Anasema neno ‘Hunijui’ limetoka kwenye uumbaji wa chorus wa Dully Sykes na kuwa na nguvu ya kubeba maudhui ya wimbo.

Huu ni mradi wake wa pili chini ya label ya Wanene Entertainment aliyosaini nayo miezi kadhaa iliyopita, baada ya ule aliomshirikisha staa wa Kenya, Khaligraph, ‘Shots’ ambao na unaendelea kufanya vizuri Afrika Mashariki. “Maendeleo ni mazuri,” anasema Young Killer kuhusiana na kuwa chini ya label hiyo maarufu nchini, nyumbani pia kwa rapper Chin Beez.

“Ni kutokana na ukweli kuwa tunafanya kazi ambayo inaonekana.”

Hunijui imetayarishwa na Bin Laden akishirikiana na Gonche na mastering kufanywa na Chizan Brain kupitia Wanene Studios. Video imeongozwa na Destro wa kampuni ya Wanene Films.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad