HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 12 June 2018

WAZIRI MKUU KUZINDUA KAMPENI YA FURAHA YANGU YA KUHAMASISHA KUPIMA VVU JUNI 19 MJINI DODOMA

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kampeni ya Furaha Yangu yenye lengo la kuhamasisha huduma za kupima UVVU na kuanza ARV mapema.

Kampeni hiyo itakayozinduliwa rasmi Juni 19 mwaka huu mkoani Dodoma inaratibiwa na  Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania(TACAIDS).

Akizungumzia uzinduzi wa kampeni hiyo leo Dar es Salaam Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Angella Ramadhan amesema kampeni ya kitaifa ya Furaha Yangu ni kampeni inayohamasisha mkakati mpya wa Serikali wa upimaji VVU na kuanza kutumia ARV mapema kwa wale watakaokutwa na VVU.

"Kupitia furaha yangu ujumbe wa Serikali ni kuwa kutambua hali yako ya VVU huleta amani, na kuanzishiwa ARV mapema kwa wale wenye VVU inawasaidia kuimarisha afya na kupunguza hatari ya kuambukiza VVU kwa wenza wao.

"Katika dira ya kuwa na Taifa bila Ukimwi, Tanzania imeridhia malengo ya UNAIDS ya 90-90-90:ambapo 90% ya watu wote wanaoishi na VVU kutambua hali zao za VVU.

"Asilimia 90 ya watu wote wenye VVU kuanza ARV, na asilimia 90 ya wote walioanza ARV kupunguza kiwango cha VVU mwilini, "amesema.

Ameongeza uzinduzi wa kampeni ya Furaha Yangu ambayo imekuwa ikiandaliwa kwa miezi kadhaa na Wizara kupitia NACP kwa kushirikiana na TACAIDS, mradi wa USAID Tulonge afya na wadau wengine ni mchango muhimu katika kutimiza malengo hayo.

"Waziri Mkuu ndio atazindua kampeni hii rasmi Juni 19 mwaka huu mkoani Dodoma ambayo pia itakuwa na siku tano za kutoa huduma za afya bila malipo ikiwemo huduma ya upimaji wa VVU kuanzia Juni 18 mwaka huu.

"Wizara kupitia NACP pamoja na TACAIDS inatoa mwito kwa wakazi wote wa Jiji la Dodoma na mikoa jirani kushiriki katika uzinduzi huu na kupima afya zao na kuonesha dhamira yao ya kumaliza VVU na Ukimwi nchini,"amefafanua.

Wakati huo huo Dk.Ramadhan ametoa shukrani kwa wanasayansia ambao wamekuwa wakiendelea kufanya tafiti kila siku zenye lengo la kuboresha utoaji huduma kwa wanaoishi na VVU.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TACAIDS Dk.Leonard Maboko ametoa ombi kwa wananchi wa makundi mbalimbali kushiriki kikamilifu katika kampeni hiyo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Kuhusu kasi ya watu kupima Ukimwi, Dk. Maboko amesema wanawake ndio wanaojitokeza zaidi kupima kuliko wanawaume na hivyo ametoa rai kwa wanaume kuhakikisha wanajenga tabia ya kupima ili wakibaini kuwa na Ukimwi waanze kutumia dawa kwa wakati.

Akizungumzia kampeni za kuhamasisha watu kupima Ukimwi amesema lugha zinazotumika kuhamasisha si za kutisha.

Ameeleza hivyo baada ya waandishi kutaka kufahamu matangazo yenye ujumbe wa kutisha yanachangia vipi kuogopesha watu kupima Ukimwi.

Ambapo amejibu kwa siku hivi mabango yenye kuzungumzia kampeni za Ukimwi hazina maneno ya kutisha akitolea mfano kampeni ya Furaha Yangu ambayo imeambatana na maneno mengine kama Pima, Jitambue, Ishi.

"Yale mabango yaliyokuwa yanasema kuwa Ukimwi unaua siku hizi hayapo tena. Hivyo mabango ya siku hizi yanamhamasisha mtu kutambua afya yake bila vitisho,"amesema Dk.Maboko.

Hata hivyo imeelezwa mbali ya kuzinduliwa mkoani Dodoma kampeni hiyo itafanyika maeno yote nchini.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dkt. Leonald Maboko, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa kampeni ya furaha ya yangu kuhamasisha huduma za kupima VVU na kuanza ARV mapema ambayo itazinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Juni 19 jijini Dodoma.
 Kaimu Mkurugenzi wa Kinga toka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Angela Ramadhani akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa kampeni ya furaha yangu ya kuhamasisha huduma za kupima VVU na kuanza ARV mapema ambayo itazinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Juni 19 jijini Dodoma.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dkt. Leonald Maboko, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa kampeni ya furaha yangu kuhamasisha ya huduma za kupima VVU na kuanza ARV mapema ambayo itazinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Juni 19 jijini Dodoma.
 Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dkt. Leonald Maboko (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni ya furaha yangu ya kuhamasisha huduma za kupima VVU na kuanza ARV mapema ambayo itazinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Juni 19 jijini Dodoma.
Naibu Mkurugenzi wa Afya toka Shirika la Misaada la Marekani (USAID) Bi. Ananthy Thambinayagan Ramadhani akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa kampeni ya furaha yangu ya kuhamasisha huduma za kupima VVU na kuanza ARV mapema ambayo itazinduliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Juni 19 jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad