HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 26 June 2018

WAZIRI MKUU AONGOZA MAADHIMISHO YA KITAIFA YA SIKU YA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA MKOANI IRINGA

Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
Watanzania wanaosafirisha dawa za kulevya nchini kwa njia mbali mbali ikiwemo ya kumeza tembe za dawa hizo tumboni kwa dhumuni ya kuzipeleka nje ya nchi au kufanyabiashara hiyo haramu ndani ya nchi wameaswa kuacha vitendo hivyo mara moja la sivyo wakikamatwa na kutiwa hatiani adhabu kali ikiwemo kifo itawakabili.

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amesema hayo leo Juni 26, 2018 wakati wa maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya duniani iliyofanyika mkoani Iringa.

Amesema, Tanzania kama mwanachama wa umoja wa mataifa haina budi kuuungana na mataifa mengine duniani kutekeleza malengo ya umoja huo ya maendeleo endelevu ili ifikapo mwaka 2030 kwa kupiga vita matuimizi na biashara hiyo haramu ili kujenga maisha yetu, jamii yetu na utu wetu bila dawa za kulevya.

Waziri Majaliwa pia amewaonya wananchi kutojihusisha kabisa na matuimizi wala biashara ya dawa za kulevya, kwani biashara hiyo haramu haikubaliki duniani na hata dini zote zinaipinga vikali, kwani kutumia dawa za kulevvya ni kujiletea laana kubwa kutoka kwa muumba.

“Ni vema tukakumbushana kuwa chini ya sheria yetu ya kuthibiti na kupambana na dawa za kulevya, adhabu yake ni kifungo cha maisha, lakini nchi nyingine kama china na Indonesia wao hutoa adhabu ya kifo, kwani wasafirishaji wengi kutoka nchi mbalimbali wameishakupamba na adhabu hiyo.

Tunapinga vita dhidi ya uhalifu wa kutisha wa dawa za kulevya ambao unatishia mustakabali wa taifa letu, napenda kusema kuua si jambo jema wala la kufurahisha lakini tufanye hivyo kwa ajili ya kuliokoa Taifa na hatari ya dawa za kulevya, hatufanyio uadui na nchi ambazo raia wake walihukumiwa kifo”, amesema waziri Majaliwa.

Ameongeza kuwa, matumizi ya dawa za kulevya yapo zaidi kwenye miji mikubwa kama Dar es Salaam Arusha, Tanga na Mwanza na kuwa matumizi hayo kwa sasa yanaenea kwa kasi kubwa kwenye miji midogo inayopitiwa na barabara kuu zinazounganisha mikoa na nchi jirani kama vile Dodoma, Iringa na Mbeya.

Amesema, hatari hiyo inafanya jamii itambue kuwa Iringa sasa ipo kwenye hatari ya kutumiwa na watu wasio waaminifu ambao huwarubuni vijana kwa kutumia au kufanya biashara ya Dawa za kulevya.

Ametoa wito kwa viongozi na watendaji wa mkoa wa Iringa kuhakikisha wanawashirikisha wananchi katika vita dhidi ya dawa za kulevya ili kuunusuru mji huo kutumiwa vibaya kma njia ya kupitisha na kufanyia biashara hiyo ya dawa haramu za kulevya.
 
Alizataja dawa za kulevya zilizobainika kutumiwa kwa wingi hapa nchini ni bangi, heroine na cocaine ambazo hutumiwa zaidi na vijana wa kuanzia umri wa miaka 15 hadi 35 ambapo utafiti uliofanywa na wizara ya afya mwaka 2014 unaonesha kuwa vijana kati ya 250,000 hadi 500,000 hutumia heroine na kati yao, vijana 300,000 hutumia dawa dawa hiyo kwa njia ya kujidunga.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa mkoa wa Iringa wakati wa maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupambana na dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika kiwanja cha Kichangani mkoani Iringa leo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipeperusha bendera aliyokabidhiwa na wananchi waliofanya matembezi ya kutoa elimu kwa wananchi yaliyofanyika kwa siku tatu mkoani Iringa wakati wa maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupambana na dawa za kulevya Duniani.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea bendera kutoka kwa wananchi waliofanya matembezi ya kutoa elimu kwa wananchi yaliyofanyika kwa siku tatu mkoani Iringa wakati wa maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupambana na dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika kiwanja cha Kichangani mkoani Iringa leo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa(katikati) akiwapungia mikono wakati alipokuwa anapokea maandamano ya wananchi pamoja na wadau mbalimbali wa kupambana na dawa za kulevya wakati wa maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupambana na dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika kiwanja cha Kichangani mkoani Iringa leo. Kulia ni Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza na kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mh. Jenista Mhagama.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa(kulia) akizungumza jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mh. Jenista Mhagama wakati wa maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupambana na dawa za ulevya Duniani yaliyofanyika katika kiwanja cha Kichangani mkoani Iringa leo.

Baadhi ya wananchi pamoja na wadau wa kupambana na dawa za kulevya wakipita kwa bashasha mbele ya mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupambana na dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika kiwanja cha Kichangani mkoani Iringa leo.Baadhi ya viongozi wa serikali na wananchi wa wa mkoa wa Iringa wakiwa kwenye maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupambana na dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika kiwanja cha Kichangani mkoani Iringa leo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Kamishna wa Sheria Edwin Kakolaki alipotembelea banda la mamlaka ya kudhibiti na kupambana na Dawa za Kulevyawakati wa maadhimisho ya kitaifa ya siku ya kupambana na dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika kiwanja cha Kichangani mkoani Iringa leo.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad