HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 26 June 2018

MTANZANIA ANAYEISHI UJERUMANI AANDAA MAFUNZO YA DANSI IJUMAA HII

Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.

Watanzania wenye vipaji wametakiwa kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza na wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika mafunzo ya kucheza yatakayoendeshwa na Mtanzania Emanuel Houston anayeishi Nchini Ujerumani.

Emanuel aliyewasili usiku wa 9 akiwa ameambatana na mkewe pamoja na wageni wengine na kupokelewa na baba yake mzazi Lusi Houston ambao kwa pamoja watatoa mafunzo ya kudansi kwa watanzania wenye vipaji.

Hii ni mara ya pili kwa Emanuel kuja nchini Tanzania kutoa mafunzo baada ya March mwaka jana kutoa elimu hiyo kwa vijana na kuonesha muitikio mzuri.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere JNIA  Emanuel  amesema kuwa anafurahi kuja Tanzania kwa mara nyingine tena kuja kutoa elimu ya dansi kwa vijana wa kitanzania na kwa mwaka huu mafunzo hayo yatakuwa kwa siku moja.

"Nafurahi kuja Tanzania kwa mara nyingine tena na kwa mwaka huu mafunzo haya yatakuwa kwa siku moja ambayo itakuwa ni Ijumaa nannawataka vijana wajitokeza kwa wingi,"amesema Emanuel.

"Mbali na kupata mafunzo hayo kwa sasa natafuta wadhamini watakaosaidiana na mimi kwani nina malengo ya kuwapatia fursa vijana watakaofanya vizuri wawili kwenda nchini Ujerumani kwa mafunzo zaidi ya kudansi, ambapo mimi nitataka wawakatie tiketi ila gharama zingine zote zitakua ni juu yangu,"amesema.

Emanuel amesema kuwa ameambatana na wanafunzi wake ambao wanadansi katika shuke yake nchini Ujerumani wenye umri takribani miaka 65 na bado wana nguvu ambapo kwa pamoja watashirikiana kutoa mafunzo hayo.

Baba mzazi Luis Houston amesema kwanza anafurahi sana wamefika salama nchini kwani yeye ni mtanzania ila ameishi miaka 40 nchini Ujerumani na bado hajasahau kuja nyumbani kutoa mafunzo hayo ambayo yana tija kwa vijana wenye vipaji.

Amesema kuwa watanzania wajitokeze kwa wingi kuja kupata mafunzi hayo kwa mwaka huu yatakayofanyika Oysterbay wakiwa na mwenyeji wao Benard Paul 'Ben Pol'.

Emanuel pamoja na baba yake wana shule ya mafunzo ya dansi nchini Ujerumani wakifundisha watu wa rika mbalimbali.
Mtanzania anayeishi Ujerumani Emanuel Houston akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ajili ya mafunzo ya dansi kwa vijana wenye vipaji nchini yatakayofanyika ijumaa.
Baba mzazi Luis Houston akizungumza na waandishi  wa habari baada ya mtoto wake Emanuel Houston (kulia) kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kwa ajili ya mafunzo ya dansi kwa vijana wenye vipaji yatakayokuwa siku ya Ijumaa.
Picha ya Pamoja ya Emanuel Houston (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na mkewe na baba yake  Luis Houston na wageni wengine waliofika kwenye mafunzo ya dansi yatakayoendeshwa Ijumaa hii.Picha na Zainab Nyamka Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad