HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 6, 2018

Watanzania watakiwa kuzikatia bima nyumba zao

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya Resolution, AnnMary Mugo akinena jambo.

Na Mwandishi Wetu

WATANZANIA wametakiwa kuzikatia bima nyumba zao ili wanufaike na fidia pindi nyumba hizo zikipatwa na majanga ya aina mbalimbali kama vile kuungua, kuharibiwa na mafuriko au majanga yoyote yale.

Mwito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bima ya Resolution, Maryanne Mugo wakati akizungumzia bima ya nyumba itolewayo na kampuni hiyo.

Alisema, jamii inatakiwa kuwa na mwamko katika kujiunga na bima hiyo ambapo malipo yake sio makubwa ikilinganishwa hasara inayoweza kutokea pindi nyumba ikikutwa na majanga mbalimbali.

Alisema,“ jamii inapaswa kutambua kuwa kuna amani na faida kubwa iwapo wakizikatia bima nyumba zao na hiyo inajidhihirisha pindi pale ambapo nyumba zikipatwa majanga iwe kuungua moto, kuvunjwa, kuharibiwa na mafuriko au majanga yoyote yale huwa bima inalipa”

Akizungumzia kuhusiana na mwamko wa watu kutumia huduma ya bima ya kampuni hiyo, alisema mpaka sasa wanao wateja 210 ambapo kati yao ni wawili tu ndo wamepatwa na majanga, mmoja ameshalipwa na mwingine anakaribia kulipwa.

Aliongeza, kuwa kuna dhana kati ya watu mbalimbali wakifikiria kuwa inachukua muda mrefu sana tangia nyumba ikipatwa majanga na kulipwa fidia ambapo alisema kwa kampuni hiyo huchukua muda mchache tu iwapo taratibu za malipo zikishakamilishwa.

Alisema, mteja hulipwa iwapo tu atakamilisha nakala muhimu kama vile ripoti ya Polisi, Makadirio ya vitu vilivyopotea au kuharibiwa ambavyo vinatokana na ripoti ya mpimaji au mkadiriaji wa bima.

“Hivi ni vitu muhimu na vya haraka vinavyotakiwa kuwakilishwa na mteja pindi nyumba yake itakapopatwa na majanga ya aina yoyote ile na kampuni za bima zinashughulikia kwa wakati”alisema.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad