HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 6 June 2018

Ecobank yafungua tawi jipya jijini Mwanza

Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa tawi jipya la Ecobank katika barabara ya Kenyatta Jijini Mwanza. Kushoto ni viongozi mbalimbali wa benki hiyo.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella amefungua tawi jipya la Ecobank Jijini Mwanza ambapo amesema benki hiyo ina nafasi kubwa ya kuchangia ukuaji wa uchumi kupitia viwanda kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa.

Amesema mikoa ya Kanda ya Ziwa ina utajiri mkubwa wa mazao, madini pamoja na viwanda hivyo benki hiyo inapaswa kushirikiana na wananchi kuchangia maendeleo ya viwanda kupitia huduma zake.

Aidha amesema mkoa wa Mwanza una fursa nyingi za uwekezaji ukiwa ni mkoa wa pili baada ya Dar es salaam kwa kuchangia pato la taifa hivyo miaka michache ijayo Mwanza itakuwa mshindani mkubwa kiuchumi na mkoa wa Dar es salaam ambapo tayari Mamlaka ya Bandari nchini inajiandaa kujenga bandari kavu katika eneo la Fella wilayani Misungwi hatua itakayosaidia uchumi wa mkoa kukua kwa kasi.

Mkurugenzi Mkuu Ecobank Tanzania, Mwanahiba Mzee amewahimiza wananchi wa Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla kujiunga na benki hiyo ili kufurahia huduma zake ambapo ina matawi saba nchini, matano Jijini Dar es salaam na mawili Arusha na Mwanza huku ikiwa na ATM mashine zenye uwezo wa kupokea VISA, Master Card, China Union, Union Pay pamoja na Pan African Card.

Awali Ecobank tawi la Mwanza lilikuwa barabara ya Karuta na sasa limehamishiwa barabara ya Kenyatta jirani na mzunguko wa samaki Jijini Mwanza ambapo Mwenyekiti wa bodi ya benki hiyo nchini Peter Machunde amesema maamuzi hayo yamelenga kuboresha huduma, kuongeza ufanisi pamoja na kuwa karibu zaidi na wateja. 
Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella akizungumza hii leo Mei 31, 2018 kwenye hafla ya uzinduzi wa tawi jipya la Ecobank katika eneo la mzunguko wa Samaki barabara ya Kenyatta Jijini Mwanza. Awali tawi hilo lilikuwa barabara ya Karuta na sasa limehamishiwa barabara ya Kenyatta ili kukidhi ili kufikisha kwa urahisi huduma bora kwa wateja.
Mkurugenzi Mkuu Ecobank Tanzania, Mwanahiba Mzee akizungumza kwenye uzinduzi huo ambapo amebainisha kwamba benki hiyo ilianzishwa mwaka 1988 katika mji wa Lome nchini Togo na hadi sasa inaongoza kwa kuwa benki kubwa barani Afrika iliyoanzishwa na Waafrika kwa ajili ya Afrika ambapo ina matawi saba nchini, matano Jijini Dar matawi mawili Arusha na Mwanza.
Mwenyekiti wa bodi ya Ecobank Tanzania, Peter Machunde akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Wanahabari Jijini Mwanza wakinasa matukio kwenye hafla hiyo.
Baadhi ya wajumbe wa bodi ya wakurugenzi Ecobank, watumishi pamoja na wateja wa benki hiyo wa Jiji la Mwanza.
Baadhi ya watendaji wa Ecobank wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa tawi la benki hiyo tawi la Mwanza.
Baadhi ya wajumbe wa menejimenti Ecobank Tanzania wakitambulishwa kwenye hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa tawi jipya la Ecobank katika barabara ya Kenyatta Jijini Mwanza. Kushoto ni viongozi mbalimbali wa benki hiyo.
Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Ecobank.
Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella (wa nne kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Ecobank. Wa pili kulia ni Mkuu wa wilaya Nyamagana Marry Tesha, nyuma ya RC Mongella ni Kamanda wa polisi mkoani Mwanza Ahmed Msangi.
Mgeni rasmi akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Ecobank.
Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella, viongozi wa Ecobank pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad