HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, 27 June 2018

Wafanyakazi wa Tume ya Utumishi wa Walimu wapatiwa mafunzo ya Mfumo wa Ofisi Mtandao (e-Office)

 Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu, Bibi Winifrida Rutaindurwa (katikati) akifuatilia mafunzo ya mfumo wa ofisi mtandao yaliyofanyika katika ukumbi wa Tume ya Utumishi wa Walimu jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi wa Ajira na Maendeleo ya Walimu, Bibi Christina Hape na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Nidhamu na Maadili ya Walimu.
  Mkuu wa Kitengo cha TEHEMA Bibi, Devota Gabriel akitoa maelezo kwa wajumbe waliohudhuria mafunzo ya mfumo wa Ofisi Mtandao.
 Mwezeshaji wa Mafunzo ya mfumo wa Ofisi Mtandandao kutoka Wakala ya Serikali Mtandao, Bw. Simba Hussein akielezea matumizi ya mfumo huo.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Ajira na Maendeleo ya Walimu, Bibi. Mectildis Kapinga (wa kwanza kushoto) akifuatilia mafunzo ya Ofisi Mtandao. Wa pili (kutoka kushoto) ni Mkuu wa Kitengo cha Mipango na Ufuatiliaji, Bw. Elia Malaki, akifuatiwa na Afisa Utumishi Mwandamizi, Bibi Shani Kamala na pembeni ni Afisa Utumishi Bw. David Igogo.
 Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mafunzo ya Ofisi Mtandao katika ukumbi wa ofisi za Tume ya Utumishi wa Walimu Dodoma.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad