HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 27, 2018

BALOZI MIGIRO AZINDUA RASMI JUMUIYA YA WATANZANIA WAISHIO UINGEREZA-ATUK

Mhe. Dkt. Asha-Rose Migiro, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za uzinduzi wa Jumuiya Mwamvuli ya Watanzania waishio nchini Uingereza na Ireland ya Kaskazini iitwayo ATUK –Association of Tanzanians in the UK zilizofanyika mjini Reading tarehe 23 Juni, 2018. Jumuiya hii inatokana na muungano wa jumuiya za diaspora kutoka mikoa mbalimbali ya hapa Uingereza na wanachama wa kujitegemea. 

Wajumbe wa Kamati ya Muda iliyoratibu kuanzishwa kwa ATUK walipongeza na kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli za kupambana na ufisadi, kusimamia uwazi na uwajibikaji katika utumishi wa umma na kuongeza kasi ya kujenga uchumi wa viwanda. Kauli mbiu ya hafla hii ilikuwa “UMOJA NI NGUVU, TANZANIA YA VIWANDA INAWEZEKANA”. Hivyo mojawapo ya malengo ya kuanzishwa kwa ATUK ni kujenga umoja na kukusanya nguvu za kuchangia jitihada za kujenga uchumi wa viwanda nchini mwetu.

Akihutubia hadhara hiyo Balozi Migiro aliwapongeza ATUK na alihimiza umoja na kukumbusha kwamba wakati wote Mhe. Rais amekuwa akisisitiza umoja wa Watanzania bila kujali tofauti zao kwani umoja ni nyenzo muhimu ya kujiteletea maendeleo. Hivyo Balozi Migiro aliwashukuru kwa Muungano huo na kueleza kwamba wakiendeleza mshikamano wataweza kuchangia kwa ufanisi jitihada kubwa za Mhe. Rais Magufuli na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuwaletea maendeleo Watanzania wote.
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Dkt. Asha-Rose Migiro akiitazama keki iliyoandaliwa wakati wa uzinduzi rasmi wa Jumuiya ya Watanzania waishio Uingereza (Association of Tanzanians in the UK-ATUK) 
Mhe. Balozi Migiro akifurahia jambo na sehemu ya Watanzania walioshiriki uzinduzi huo 
Sehemu ya Watanzania na wageni waalikwa waliohudhuria tukio hilo la kihistoria 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad