HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 25 June 2018

Utafiti wa miaka 6 wa uwezeshaji kiuchumi kama sehemu ya uzazi wa mpango wakamilika

Na Mwandishi wetu
TAASISI ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shule ya Uchumi ya Norway (NHH) umekamilisha utafiti uliochukua miaka sita uliopelemba kama uwezeshaji wasichana kiuchumi ndio njia ya kuwezesha uzazi wa mpango.
Matokeo ya utafiti huo ‘Girls’ Economic Empowerment: The Best Contraceptive?’ umeelezwa kuja kusaidia kuelewa uzazi kwa wasichana na athari ya hali hiyo katika maamuzi yao ya kiuchumi.
Utafiti huo uliofanywa kuanzia mwaka 2013 hadi 2018, ulifanywa kufuatia programu iliyotengenezwa na Femina Hip, taasisi inayojishughulisha na kubadili tabia za vijana kwa kutumia mawasiliano.
Katika programu hiyo wasichana wa sekondari walipewa mafunzo ya ziada nje ya utaratibu wao yaliyochanganywa na elimu ya afya ya uzazi, uwezeshaji kiuchumi na elimu ya maisha.
Ubalozi wa Norway jijini Dar es salaam ulifadhili sehemu ya programu hiyo.
 Maarifa yaliyopatikana kutokana na utafiti huo yanatarajiwa kuwasaidia watengeneza sera, wanazuoni na  watu wa asasi zisizo za kiserikali kutambua athari za kuwezesha au kutowezesha wasichana kiuchumi katika uzazi.
Lengo kuu la utafiti huo ni kuwa na uelewa mpana utakaowezesha uundaji wa sera stahiki kuhusu uchumi na uzazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF Dk Tausi Kida alisema kwamba amejisikia furaha sana kufanyakazi na  Shule ya Uchumi ya Norway, ubalozi wa Norway na Femina katika kutafuta suluhu kwa matatizo yanayokabili taifa.
Alisema kwamba tabia, maarifa, ujuzi na maamuzi kwa vijana kuhusu afya yao ya uzazi kuna athari kubwa kwa maendeleo na afya kwa ujumla.
Imeelezwa kuwa wakati wa kuanza kwa utafiti huo, kundi la utafiti lilionesha kwamba hali ya kimaskini waliyokuwa wanakabiliana nayo iliwafanya wajihusishe na ngono.
Utafiti ulibaini kwamba kuwasaidia wasichana kabla ya ndoa kunawapa fursa zaidi za kukua kiuchumi.
Pia  umeonesha kwamba mafunzo ya afya yalifanya wasichana kutafuta mahusiano yenye uhakika na hivyo kuwa na athari chanya katika afya.
Matokeo ya awali ya utafiti yanaonesha kwamba mafunzo hayo yamesaidia sana kuwafumbua wasichana ambao walionesha wazi kwamba inasaidia kutambua masuala yao ya mapenzi na masuala ya kiuchumi.
Katika utafiti huu Femina-Hip ilipeleka programu hiyo kwa wasichana 6000 katika maeneo mbalimbali ya Tanzania na kuleta matokeo yanayoonesha kwamba kufunza wasichana elimu ya maisha, afya ya uzazi, fedha na masuala ya uanzishaji biashara kuna wafanya wajiamini zaidi katika safari ya kutafuta kuwa huru kifedha.
Mkurugenzi wa Vyombo vya habari wa Femina Hip, Amabilis Batamula alisema kwamba utafiti huo unaonesha kwamba wanawake wakiwa wanajiweza kifedha wanakuwa na nguvu na uwezo wa kuamua kuhusu masuala yao ya uzazi.
Akizungumza katika tukio hilo Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne-Marie Kaarstad, alielezea umuhimu wa kuwawezesha wasichana ili kutambua haki zao na kuzitumia ipasavyo.
Alisema nchi yake itaendelea kuisaidia Tanzania katika kuhakikisha usawa wa kijinsia moja kwa moja au kupitia mashirika ya Umoja wa Mataifa ikiwamo UNDP.
Wakati huo huo serikali imeelezea kuridhishwa kwake na utafiti huo ambao imesema utawasaidia katika kutengeneza sera nzuri zaidi za kuwawezesha wanawake vijana katika kujitambua na kushiriki vyema katika uchumi wa taifa.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi msaidizi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Wanawake Jinsia Watoto na Wazee (jinsia), Mboni Mgaza.
Akifungua kongamano hilo la utoaji wa matokeo hayo ya utafiti alisema pamoja na kuwapo kwa sera za kusaidia afya ya uzazi kwa vijana ya mwaka 2011 na 2016 bado kuna wimbi kubwa la upatikanaji wa mimba na hivyo anaamini matokeo hayo ya utafiti yatasaidia watengeneza sera kuelewa mahitaji halisi ya wanawake vijana.
Alisema takwimu za sasa kuhusiana na mimba kwa watoto wa shule na pia kuwapo kwa wazazi vijana na suala la umaskini hazitoi taswira nzuri na hivyo kushukuru wafadhili wa utafiti na waliofanya utafiti kwa kuja na majawabu kutoka miongoni mwa wanajamii wenyewe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida (kushoto) akimsikiliza Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne-Marie Kaarstad (wa kwanza kulia) mara baada ya kuwasili ofisini kwake kwa mazungumzo wakati wa mkutano wa kujadili matokeo ya utafiti wa uwezeshaji wasichana kiuchumi kama njia ya uzazi wa mpango uliofanyika mwishoni mwa wiki ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Mkurugenzi msaidizi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Wanawake Jinsia Watoto na Wazee (jinsia), Bi.Mboni Mgaza.
Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne-Marie Kaarstad akisalimiana Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Bi. Jacqueline Mohan pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) huku Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida (kushoto) akisalimiana na wageni waalikwa wakati wa mkutano wa kujadili matokeo ya utafiti wa uwezeshaji wasichana kiuchumi kama njia ya uzazi wa mpango uliofanyika mwishoni mwa wiki ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene (kulia) akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk Tausi Kida (kushoto) pamoja na Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne-Marie Kaarstad (kaitkati) kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF wakati wa mkutano wa kujadili matokeo ya utafiti wa uwezeshaji wasichana kiuchumi kama njia ya uzazi wa mpango uliofanyika mwishoni mwa wiki ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa wadau na wageni waalikwa wakati wa mkutano wa kujadili matokeo ya utafiti wa uwezeshaji wasichana kiuchumi kama njia ya uzazi wa mpango uliofanyika mwishoni mwa wiki ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi msaidizi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Wanawake Jinsia Watoto na Wazee (jinsia), Bi. Mboni Mgaza akisoma hotuba ya ufunguzi wa mkutano wa kujadili matokeo ya utafiti wa uwezeshaji wasichana kiuchumi kama njia ya uzazi wa mpango uliofanyika mwishoni mwa wiki ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne-Marie Kaarstad akizungumza jambo wakati wa mkutano wa kujadili matokeo ya utafiti wa uwezeshaji wasichana kiuchumi kama njia ya uzazi wa mpango uliofanyika mwishoni mwa wiki ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Vyombo vya habari wa Femina Hip, Amabilis Batamula akielezea jinsi Femina Hip kupitia program hiyo ilivyoweza kufikia wasichana wakati wa mkutano wa kujadili matokeo ya utafiti wa uwezeshaji wasichana kiuchumi kama njia ya uzazi wa mpango uliofanyika mwishoni mwa wiki ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Profesa kutoka Shule ya Uchumi ya Norway (NHH),  Kjetil Bjorvatn akiwasilisha matokeo ya utafiti wa uwezeshaji wasichana kiuchumi kama njia ya uzazi wa mpango uliofanyika mwishoni mwa wiki ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Kutoka kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez,  Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hanne-Marie Kaarstad, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida pamoja na Mkurugenzi msaidizi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Wanawake Jinsia Watoto na Wazee (jinsia), Bi. Mboni Mgaza wakimsikiliza Mshehereshaji wa mkutano wa kujadili matokeo ya utafiti wa uwezeshaji wasichana kiuchumi kama njia ya uzazi wa mpango Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene uliofanyika mwishoni mwa wiki ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.


  Sehemu ya washiriki kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wa jinsia na serikalini walioshiriki kwenye mkutano wa kujadili matokeo ya utafiti wa uwezeshaji wasichana kiuchumi kama njia ya uzazi wa mpango uliofanyika mwishoni mwa wiki ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
 Shemu ya washiriki kutoka taasisi mbalimbali wakishiriki kuchangia maoni wakati wa mkutano wa kujadili matokeo ya utafiti wa uwezeshaji wasichana kiuchumi kama njia ya uzazi wa mpango uliofanyika mwishoni mwa wiki ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida akifurahi jambo katika picha ya kumbukumbu na baadhi ya wageni waalikwa mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa kujadili matokeo ya utafiti wa uwezeshaji wasichana kiuchumi kama njia ya uzazi wa mpango uliofanyika mwishoni mwa wiki ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad