HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 25 June 2018

TBL kuiona Liverpool live EPL baada ya kutwaa kombe la Standard Chartered 2018

Na Mwandishi wetu
Timu ya soka ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) imetwaa kombe la benki ya Standard Chartered baada ya kuitandika kwa mikwaju ya penalti  2-1 timu ya Mwananchi Communications Limited .
Kwa ushindi huo, timu ya TBL sasa itakuwa na ziara ya siku 3 nchini Uingereza na kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa ya Standard Chartered yaliyopangwa kufanyika kwenye uwanja wa Anfield, Septemba mwaka huu.
Aidha timu hiyo ya TBL wakifika Anfield wataona mechi ya msimu mpya wa EPL mubashara na kuzungumza na magwiji na kupata nafasi ya kunolewa nao.
Katika michuano hiyo Mchezaji wa Mwananchi, Saidi Seif alifunga mabao manane na kuwa mfungaji bora.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe na gwiji la timu ya Liverpool, Sami Hyypia walishuhudia mechi hiyo na kutoa zawadi kwa washindi.
Akizungumza mara baada ya mashindano hayo kumalizika, Dk Mwakyembe aliipongeza timu ya TBL kwa kutwaa ubingwa na kuishukuru benki ya Standard Chartered kwa kutoa mchango wake kukuza sekta ya michezo.
“Naipongeza benki ya Standard Chartered kwa kuendesha mashindano haya na kuleta hamasa katika soka, nimefarijika sana na nimeshuhudia vipaji vingi, soka ina wigo mpana na ninaamini tunaweza kufanya vyema katika mashindano mbalimbali kwa kutumia vipaji vyetu,” alisema Dk Mwakyembe.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani alisema kuwa benki yao ni wadau wakubwa wa maendeleo ya michezo nchini na katika sekta nyingine na kuahidi kuendelea kufanya hivyo kwa maendeleo ya taifa.
Rughani alisema kuwa wamefarijika sana kuendesha mashindano kutokana na kupata ushirikiano mkubwa kutoka Shirikisho la soka nchini, TFF na serikali.
Katika msimu huu Meneja Uhusiano na Masoko wa benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba amesema kwamba benki yake inafuraha kuendelea kusaidia kukuza vipaji vya vijana nchini kwa kutumia magwiji wa Liverpool.
Alisema benki yake ni wadhamini wa timu hiyo na wamekuwa wakihakikisha kwamba wanashirikiana kukuza vipaji katika nchi ambazo benki inafanyabiashara zake.

Alisema mwaka jana walimleta John Barnes ambaye pia aliendesha kliniki ya soka hali ambayo inaimarisha utaalamu na kisaikoilojia kwa vijana.
Alisema ni lengo la benki hiyo kuhakikisha kwamba wanawalea wataalamu  kuboresha vipaji vya soka kukua nchini.
Kukamilika kwa fainali hizo zilizoshirikisha timu 32, pia kunahitimisha ziara ya veteran wa timu ya soka ya Uingereza ya Liverpool, Sami Hyypia ambaye akiwa nchini aliwataka vijana Watanzania kuongeza bidii katika kuhakikisha kwamba wanafikia hatua za juu za uchezaji soka hivyo kupata nafasi ya kucheza Ulaya.
Alisema hayo wakati wa kiliniki ya soka aliyoifanya kwa vijana wa Serengeti boys alipokuwa akishiriki nao katika mafunzo na mazoezi.
Alisema kwamba yeye hakuwa na kipaji kikubwa kuliko alivyoviona kwa vijana hao lakini ameweza kufikia hatua za juu kabisa za uchezaji wa soka kutokana na kujituma kwake.
Alisema amewaambia vijana kuangalia zaidi juhudi kwani kipaji pekee hakitoshi kumfanya mtu kuwa gwiji katika soko.
Alisema pamoja na mafundisho ya walimu ni kazi ya mchezaji mwenyewe kuona udhaifu wake uliopo na kuufanyia kazi ili aweze kuwa mwanasoka bora wa kutregemewa.
Amesema siri kubwa ya mafanikio ni kujituma kwa mchezaji pamoja na kwmaba anakipaji na walimu wazuri.


 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe (wa pili kulia) akiongozana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (wa pili kushoto), Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye mashindano ya kombe la benki ya Standard Chartered yaliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe (kulia) akimpongeza Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia (wa pili kushoto) kwa kuja nchini kushuhudia mashindano ya kombe la benki ya Standard Chartered yaliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi (kushoto).
 Kapteni wa timu ya kampuni ya Mwananchi Communications Limited, Majuto Omary (katikati) akimtambulisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe (kushoto) kwa kikosi cha timu hiyo wakati wa fainali kati ya TBL na MCL katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
 Kapteni wa timu ya kampuni ya TBL akimtambulisha Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe kwa kikosi hicho baada ya kutinga fainali za mashindano ya kombe la Standard Chartered yaliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani akisalimiana na kikosi cha timu ya TBL kabla ya kukipiga kwenye fainali za mashindano ya kombe la Standard Chartered yaliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
 Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia akisalimiana na kikosi cha timu ya kampuni ya TBL kabla ya kuanza mchezo wa fainali na timu ya Mwananchi Communications Limited wakati wa mashindano ya kombe la Standard Chartered yaliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe, Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia, Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani katika picha ya pamoja na timu zilizotinga fainali mashindano ya kombe la benki ya Standard Chartered yaliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.

 Wachezaji wa timu ya TBL (kijani) na Mwananchi Communications Limites (nyeupe) wakimenyana katika fainali za mashindano ya kombe la benki ya Standard Chartered yaliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
 Wadau kutoka makampuni mbalimbali wakitazama mechi ya timu zilizoingia fainali kwenye mashindano ya kombe la benki ya Standard Chartered yaliyofanyika katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
 Timu ya soka ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ikisherehekea ubingwa wa kombe la benki ya Standard Chartered baada ya kuitandika kwa mikwaju ya penalti  2-1 timu ya Mwananchi Communications Limited katika mashindano yaliyofanyika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
 Kapteni wa timu ya kampuni ya Mwananchi Communications Limited, Majuto Omary akisalimiana na Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia wakati akielekea kukabidhiwa medali na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe katika mashindano ya kombe la benki ya Standard Chartered yaliyofanyika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akiwavalisha medali kikosi cha kampuni ya TBL baada ya kuibuka mabingwa wa mashindano ya kombe la benki ya Standard Chartered yaliyofanyika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani kwa pamoja wakikabidhi kombe kwa kapteni wa kampuni ya TBL mara baada ya kutwaa ubingwa wakombe la benki ya Standard Chartered baada ya kuitandika kwa mikwaju ya penalti  2-1 timu ya Mwananchi Communications Limited katika mashindano yaliyofanyika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
 Mabingwa wa mashindano ya kombe la benki ya Standard Chartered kampuni ya Bia ya TBL wakishangilia mara baada ya kukabidhiwa kombe hilo wakati mashindano hayo yalipofikia tamati mwishoni wa wiki katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
 Mabingwa wa mashindano ya kombe la benki ya Standard Chartered kampuni ya Bia ya TBL wakifurahia na kubusu kombe lao mara baada ya kuibuka mabingwa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 yalipofikia tamati mwishoni wa wiki katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
 Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani, Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia pamoja na Mkurugenzi wa Ufundi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi wakiwa kwenye picha ya pamoja na mabingwa wa kombe la Standard Chartered 2018 yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani akiteta jambo na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered nchini, Juanita Mramba mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumaliza zoezi la kukabidhi kombe kwa mabingwa wa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 yaliyomalika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Gwiji la soka, klabu ya Liverpool, Sami Hyypia.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered nchini, Sanjay Rughani akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya kombe la Standard Chartered 2018 viwanja  vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad