HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, June 29, 2018

UBALOZI WA TANZANIA NCHINI URUSI WATOA SOMO KWA WAMILIKI WA KAMPUNI YA UTALII NCHINI HUMO

BALOZI wa Tanzania nchini Urusi, Meja Jenerali Simon Mumwi leo ameendesha semina kwa wamiliki wa kampuni za uandazi wa ziara za  watalii (Tour Operators) jijini Moscow ili kuwapa ufahamu wa vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini Tanzania.

Semina hizo ambazo hufanyika mara moja kila mwezi, zinalenga kuongeza idadi ya watalii kutoka Urusi na nchi za jirani wanaotembelea Tanzania.

Akizungumza katika hafla hiyo, Balozi Mumwi alisema kuwa semina hizo zimekuwa na manufaa makubwa kwani katika kipindi kifupi zimesaidia sana kuongeza idadi ya watalii wanaotoka Urusi kwenda nchini Tanzania, ambapo alisema "katika kipindi cha miaka 10, idadi ya watalii kutoka Urusi imeongezeka kutoka 1,500 mpaka 15,000 mwishoni mwa mwaka 2015."
Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Meja Jenerali Simon Mumwi akizungumza wakati akifungua semina ya siku moja ya kuhamasisha utalii wa Tanzania nchini Urusi, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Ubalozi, 51 Ulitsa Bolshaya Nikitskaya, Jijini Moscow, nchini Urusi. wanufaika wa semina hiyo walikuwa ni waendeshaji wa ziara za Utalii kutoka nchini Urusi.
Afisa Mawasiliano wa Ubalozi wa Tanzania nchini Urusi anayeshughulia pia maswala ya Utalii, Biashara na Uwekezaji, George Lengeju akieleza jambo kuhusiana na vivutio mbalimbali vilivyopo nchini Tanzania, katika semina ya siku moja kwa wamiliki wa kampuni za uandazi wa ziara za watalii (Tour Operators) nchini Urusi, iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Ubalozi, 51 Ulitsa Bolshaya Nikitskaya, Jijini Moscow.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Safari ambaye ndiye aliyewezesha kuwakutanisha wadau wa masuala ya utalii nchini Urusi, Galina Modestova akizungumzia vivutio mbalimbali vilivyopo nchini Tanzania kwa lugha ya kirusi.
Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Meja Jenerali Simon Mumwi akifuatilia mada ya utalii nchini Tanzania, iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Safari ambaye ndiye aliyewezesha kuwakutanisha wadau wa masuala ya utalii nchini Urusi, Galina Modestova (kushoto) aliyekuwa akiwasilisha mada hiyo kwa lugha ya kirusi.
Sehemu ya wamiliki wa kampuni za uandazi wa ziara za watalii (Tour Operators) wakipitia vipeperushi mbalimbali vya utalii wa Tanzania, wakati wa semina hiyo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Ubalozi, 51 Ulitsa Bolshaya Nikitskaya, Jijini Moscow, nchini Urusi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad