HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, 29 June 2018

KAMPENI YA “MIAKA 20 YA KUJALI JAMII” YA BENKI YA EXIM YAFIKA KILIMANJARO

Mkuu wa idara ya masoko na mwasiliano wa benki ya Exim Tanzania, Stanley Kafu  akiongea katika halfa ya makabidhiano ya vitanda na magodoro 50 kwa hospital ya mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi kama sehemu ya mradi wa benki hiyo ya miaka 20 ya kujali jamii.
  
 Mganga Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Best Magoma akitoa shukrani kwa Mkuu wa idara ya masoko na mawasiliano wa Benki ya Exim Tanzania kwenye halfa ya makabidhiano ya vitanda na magodoro 50 kwa hospital ya mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi kama sehemu ya mradi  wa benki hiyo ya miaka 20 ya kujali jamii.

  BENKI ya Exim Tanzania leo imekabidhi vitanda na magodoro 50 kwa Hospitali ya mkoa ya Mawenzi, mkoani Kilimanjaro. Benki ya Exim Tanzania iliadhimisha miaka 20 ya huduma, mwezi wa Agosti mwaka jana, kwa kuzindua mradi wa mwaka mzima unaoitwa “miaka 20 ya kujali jamii” ambao Benki hiyo itawekeza katika sekta ya afya Tanzania hasa kwenye kuboresha huduma za afya zinazotolewa kwa wakina mama na wanawake.
Hospitali na kliniki nyingi nchini zina tatizo la ukosefu wa dawa, vifaa na vitanda hasa katika hospitali za rufaa. Katika kukabiliana na uhaba huu unaosumbua taifa, benki ya Exim Tanzania, yenye uwepo wa kimataifa imeanzisha mradi unaolenga kusaidia upungufu wa vitanda katika wodi za wazazi kwenye hospitali nchini - hivyo benki ya Exim itatoa magodoro and vitanda 500 katika hospitali za serikali katika mikoa 13 nchini kama sehemu ya kampeni yake ya mwaka yenye lengo la kusherehekea miaka 20 ya kutumikia jamii.

Hospitali ya Mawenzi mkoani Kilimanjaro ni hospitali ya kumi na moja kupokea mchango huu baada ya hospitali ya serikali ya Sekou Toure ya mkoani Mwanza mwezi uliopita, hospitali ya rufaa ya Morogoro mwezi Aprili, hospitali ya rufaa ya Mwananyamala mkoani Dar es Salaam mwezi Machi, hospitali  ya rufaa ya Bombo, mkoani Tanga mwezi Febuari, hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mbeya mwezi Januari, hospitali ya Mount Meru, Arusha mwezi Desemba, Hospital ya rufaa Dodoma mwezi Novemba, hospitali ya rufaa Ligula, Mtwara mwezi Oktoba, Hospitali ya Mnazi Mmoja, Unguja, Zanzibar mwezi Septemba na Hospitali ya rufaa Temeke, Dar es Salaam mwezi wa nane mwaka jana. Tukio lilifanyika kwenye hospitali hiyo katika wodi ya wazazi na mgeni rasmi alikuwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dr. Best Magoma. 

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Best Magoma alipongeza Exim Bank Tanzania kwa msaada wake na kuhimiza taasisi mbalimbali kutekeleza ishara ya Benki ya Exim Tanzania katika kusaidia kuboresha huduma ya afya kwa nchini. Aliongezea kwa kusema “Upungufu wa vitanda katika mahospitali ni changamoto kubwa. Msaada huu kutoka benki ya Exim wa hivi vitanda 50 na magodoro utasaidia sana katika kupunguza changamoto hii .”

Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano, Mkuu wa idara ya masoko na mawasiliano wa benki ya Exim, Stanley Kafu alisema, “Benki imetambua umuhimu wa jumuiya zinazozunguka eneo la biashara yetu na ndio maana shughuli za kijamii ni muhimu sana kwa Benki ya Exim. Tunaamini kwamba tuna sehemu kubwa katika kufanya mabadiliko mazuri katika sekta mbalimbali katika jamii zetu. Ni kwa hili Benki iliamua kusherehekea miaka 20 kwa kusaidia jamii kwa njia ya kampeni inayoitwa, “miaka 20 ya kujali jamii” kuonyesha jinsi tunavyowashukuru. Benki ya Exim itatoa vitanda na magodoro ya hospitali kwa hospitali nchini kote kila mwezi kwa mwaka mzima”.

Ikiwa kama sehemu ya mradi wa “miaka 20 ya kujali jamii” benki ya Exim itatoa msaada wa vitanda 500 na magodoro yake kwa hospitali katika mikoa ya Mwanza, Morogoro, Tanga, Dodoma, Kigoma, Kilimanjaro, Mbeya, Arusha, Shinyanga, Mtwara, Dar es Salaam, Pemba na Unguja.
Benki ya Exim ilitambuliwa kama benki bora kwa huduma ya wateja binafsi mwaka 2017 inasheherekea miaka 20 ya mafanikio, ukuaji na kuwa kiongozi katika kuingia katika masoko mapya barani Afrika. Benki ya Exim ilianzishwa mwaka 1997 na imetanua soko lake kwa kufungua kampuni tanzu katika nchi za Comorro (2007), Djibouti (2010) na Uganda (2016).

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad