HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, June 11, 2018

TRC WAPEWA MIEZI MITATU KUWEKA VIZUIZI MAENEO YOTE AMBAYO RELI INAKATIZA BARABARA ILI KUEPUKA AJALI

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii

SHIRIKA la Reli Tanzania(TRC) limepewa muda wa miezi mitatu kuhakikisha maeneo yote ambayo reli inakatiza barabara kuwe na vizuizi  badala ya kutegemea alama peke yake.
Uamuzi huo unakuja ikiwa ni siku chache zimepita  tangu kutokea kwa ajali ya basi kugonga treni mkoani Kigoma na kusababisha watu 10 kufariki dunia na wengine 26 kujeruhiwa.
Maagizo hayo yametolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati anazindua bodi mpya ya wakurugenzi ya TRC.
Hivyo wakati anazungumza na wajumbe hao na watumishi wa TRC amesema ipo haja ya kuweka vizuizi kwenye maeneo ambayo reli inakatiza barabara.

Amesema katika suala la usalama wa raia wa nchi hii gharama isiwe kigezo cha kutowekwa vizuizi hivyo huku akitoa maagizo ndani ya miezi mitatu kuanzia sasa vizuizi viwe vimewekwa.
"Hakikisheni kunakuwa na vuzuizi kwenye maeneo ambayo reli inakatiza barabara, ile ajali ya Kigoma kama kungekuwa na kizuizi huenda isingetokea.

"Kuwa na alama peke yake haitoshi kwani wapo wengine macho yao hayaoni mbali, hivyo kukiwa na kizuizi hakuna anayeweza kupita,"amefafanua Waziri Mbarawa.

Amesema vizuizi hivyo vinaweza kuwa vya nguzo ambapo kutakuwa na mtu maalum atatakiwa kukaa na hata akilipwa Sh.300,000 kwa mwezi si mbaya na wala si gharama mbele ya uhai wa mtanzania, hivyo vizuizi hivyo vianze kuwekwa mara moja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad