HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 25 June 2018

TAMASHA LA ASAS MTOTO DAY OUT KUFANYIKA JUNI 30 DAR KWA KIINGILIO CHA 5000/-*Ni tamasha maalum kwa watoto, lashesheni michezo ya kila aina kwa watoto

TAMASHA la Mtoto Day Out ambalo limebeba jina la Asas Mtoto Day Out linatarajia kufanyika Juni 30 mwaka huu katika Viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam kwa kiingilio cha Sh.5000 tu.

Imefahamika kuwa mtoto atacheza michezo ya kila aina huku mzazi akiingia bure huku ikifafanuliwa Mtoto Day Out ni tamasha kwa ajili ya watoto kukutana kwa wingi kucheza na kufurahi pamoja.

Akizungumzia leo jijini Dar es Salaam Mratibu wa tamasha hilo Dina Marious amesema tamasha hilo litawapa nafasi watoto kucheza michezo ya kila aina na kuonesha vipaji, huku wakijishinidia zawadi mbalimbali. 

"Moja ya haki za watoto ni kucheza na katika kucheza hujifunza mambo mbalimbali.Michezo kwa watoto isiwe kero kwa mzazi bali nafasi ya mtoto kujifunza na kuchangamsha akili yake."Katika michezo kuna michezo ya kushindana ambayo ni jambo jema kwa watoto kupanda ndani yao ari ya ushindani hata katika maisha ya baadae."Wazazi kawaida wana Outing zao za kikubwa na watoto huishia mara moja moja kupelekwa kwenye michezo,"amesema,

Ameongeza kupitia tamasha la Mtoto Day Out wanataka liwe tamasha la watoto kama ambavyo watu wazima wana matamasha yao na kufafanua "unapotoka na mtoto wako kuja Mtoto Day Out unamtoa yeye Out si wewe".Amesema kuwa hiyo ni mara ya tatu kwa tamasha hilo kufanyika na kufafanua tamasha la safari hii litafanyika Viwanja vya Posta Kijitonyama Sayansi jijini.Muda wa kuanza kwa tamasha hilo ni kuanzia saa nne asubuh mpaka saa 12 jioni na kutakuwa na michezo ya kila aina kwa watoto.

Baadhi ya michezo hiyo ni jumping castles, face painting, train, magari ya kuendesha,climber,mabembea,swimming pools,water slides,football arena na sarakasi.Marious amesema pia kutakuwa na kona ya michezo ya watoto wadogo wa mwaka hadi miaka 3, kona ya watoto kusoma vitabu na kuchora.Pia atakuwepo Mchekeshaji Mpoki ambaye atasasherehesha watoto huku msanii Msami akiwachezesha watoto. Katika tamasha hilo vyakula uwanjani vitakuwepo na wazazi watawanunulia watoto kwa bei nafuu kabisa.

"Tamasha hili linafanyika kwa udhamini wa Asas_dairies, Finca microfinance bank,majibora, ara juice, bagtriks, swahilifastfood,saloon ya watoto ya kiddieskingdomtz,dinamarios coconut baby oil, efmtanzania na tvetanzania ."Tunapenda kuwakaribisha wazazi na watoto kutakuwa na timu kubwa ya kuangalia watoto kwa kushirikiana na wazazi.
Mratibu wa tamasha la ASAS Mtoto Day Out Dina Marios akizungumza mapema leo mbele ya Waandishi wa habari kuhusu tamasha hilo,linalotarajia kufanyika Juni 30 mwaka huu katika Viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam,ambapo kiingilio kimetajwa kuwa ni Sh.5000 tu,Pichani kulia ni Mmoja w Waratiu wa tamasha hilo Glory Shayo na kushoto ni Meneja Masoko wa kampuni ya ASAS Jimmy Kiwelu.
Mkutano huo ukiendelea na Waandishi mapema leo jijini Dar 
Balozi wa ASAS Mujuni Sylivery maarufu kwa jina la Mpoki akiwaonesha Waandishi wa Habari baadi ya bidhaa zinazotengenezwa na kampuni hiyo,huku akiwashauri wazazi kuhakikisha wanawapa furaha watoto wao kwa kuwapeleka kwenye tamasha hilo ambapo amewahakikishia amejiandaa vema kwa ajili ya kuwafurahisha. 
Meneja Masoko wa ASAS Jimmy Kiwelu akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar,kuhusu kukamilika kwa maandalizi ya tamasha la Asas Mtoto Day Out,Kiwelu amesema wanatambua umuhimu wa watoto kushiriki kwenye michezo mbalimbali, hivyo wakaona iko haja ya wao kuhakikisha tamasha hilo linafanikiwa ili kuwapa nafasi watoto kukutana na kucheza kwa pamoja.Amesema Asas siku zote wamekuwa wakiamini katika kuhakikisha mtoto anakuwa na furaha kwani furaha ya mtoto ndio furaha kwa mzazi/mlezi. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad