HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 11 June 2018

STARTIMES TANZANIA SASA WAJA NA STARTIMES APP KUELEKEA KOMBE LA DUNIA

Katika msimu wa Soka ambapo kila mpenzi wa Soka duniani anayo matarajio makubwa na timu anayoishabikia, StarTimes inakuletea Ofa Kabambe ya Damka na StarTimes App ambapo mteja atapata Michuano ya Kombe la Dunia kwa shilingi 3500 tu atakapotumia StarTimes App inayopatikana PlayStore kwa watumiaji wa Android na AppStore kwa watumiaji wa IOs (Iphone).

Kampuni ya StarTimes ndiyo kampuni ya kwanza Tanzania kuleta mapinduzi ya kidigitali na hii sasa inakuwa ni hatua nyingine kuelekea Mapinduzi mapya kwa teknolojia ya vipindi kwa njia ya simu. Na kwa msimu huu wa Kombe la Dunia wateja na wasio wateja wa StarTimes kwa pamoja wanaweza kuangalia michuano hiyo kwa gharama nafuu kabisa ya Tsh. 3500 tu kupitia StarTimes App.

Akiongea katika Uzinduzi wa huduma hiyo, Meneja Masoko wa StarTimes Ndg. David Malisa alisema, “Ni wazi wengi wetu tumeshuhudia jinsi ambavyo gharama za Internet ziko ghali hasa unapotaka kufanya “Live Streaming”. Kwa kupitia teknolojia ya App yetu, wateja wetu watatumia kiasi kidogo sana cha data. Huu ndio wakati wa kwenda kidigitali zaidi Pakua App yetu sasa, kuwa miongoni mwa wateja 20,000 wa kwanza kujiunga na StarTimes App na utalipia 3500 tu”.

“Kwa 3500 hiyo utapata mechi zote 64 MUBASHARA kiganjani mwako tena kwa Siku 38, kwa kiwango cha screen utakachopenda wewe iwe SD, HD au Ultra-High Definition (UHD) chaguo ni lako. Baki na Sisi Soka limenoga”. Aliongezea Ndg. Malisa.

Ofa hii ni kwa wateja 20,000 tu watakaopakua StarTimes App kabla ya tarehe 14 Juni yaani Alhamisi ya wiki hii. Kombe la Dunia linaanza siku hiyo hiyo ya Alhamisi ambapo StarTimes ni mrushaji rasmi wa michuano hiyo inayofanyika nchini Russia.
Meneja wa Masoko na Matangazo wa StarTimes, David Malisa akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa kampeni ya Tukio Kubwa Zaidi la Soka Duniani. Mashabiki wa soka sasa wanaweza kutazama mechi za Kombe la Dunia laivu kwenye simu zao za mkononi kupitia Star Times App
Afisa wa Habari wa StarTimes, Sam Gisayi akionesha hatu aza kujiunga na huduma mpya ya StarTimes App itakayowezesha wapenzi wa soka kutazama mechi zote 64 za kombe la Dunia laivu kwenye simu zao za mkononi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad