HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 23 June 2018

RC PWANI AWAAGIZA TBS KUFANYA ZIARA ZA KUSHTUKIZA KWENYE MADUKA YA BIDHAA MBALIMBALI ILI KUDHIBITI UBORA


Na Linda Shebby,  Kibaha Pwani


MKUU wa Mkoa wa Pwani Injinia Everist Ndikilo amewataka  uongozi wa Shirika la Viwango nchini (TBS), kutokukaa maofisini na kusubiri wafanya biashara wawapelekee bidhaa zao wanazozizalisha kwani wanaweza kufanya udanganyifu hivyo kuweza kujipatia sifa ya ubora ambao hawakustahili.Mheshimiwa Ndikilo amesema kuwa anategemea kuona bidhaa zinazozalishwa  na viwanda  vya Mkoa wa Pwani  na nchi  nzima kwa ujumla ziwe vinakidhi viwango vya ubora  unaostahiki kwa kuzalisha  bidhaa bora  na zitakazoweza kuleta ushindani kwenye masoko yetu yote ya ndani na nje ya nchi.Amesema  kuwa ili kuitekeleza  azma   ya Uchumi wa Viwanda  kwa ukamilifu  ametoa rai kwa  wenye viwanda  na wazalishaji  nchini kote  kuzalisha bidhaa kwa kutumia  vipimo stahiki  ili kuweza kukidhi vigezo vya kitaifa na kimataifa na  kuweza kungia  kwenye  ushindani wa masoko ya Kimataifa.Mheshimiwa Ndikilo amesema kuwa  pamoja na juhudi zinazofanywa na  Shirika la Viwango Tanzania (TBS) bado kunachangamoto nyingi kama vile umbali mrefu kutoka ofisi za Kanda hadi Mkoa na hivyo kusababisha baadhi ya  wafanyabiashara kushindwa kupata huduma kwa urahisi, huku upimaji huo umekuwa ukichukua muda mrefu hali inayosababisha  kuendelea kuzalisha  bidhaa zisizo na uthibitisho.Hivyo amewataka TBS kufungua matawi ya ofisi zao kwenye Mikoa ikiwa ni katika kurahisisha huduma zao kwani zitasaidia kupunguza gharama  kwa wafanyabiashara kwa lengo la kuongeza  ubora wa bidhaa.Mkuu huyo wa Mkoa wa Pwani amesema hayo  wakati alipokua akifungua  ,mafunzo ya vipimo ya  siku moja yaliyokwenda sambamba na  maadhimisho ya siku ya Vipimo Duniani ambayo yameadhimishwa Mkoani Pwani leo.Huku katika  historia siku hii ya vVpimo Duniani huadhimishwa kila ifikapo Mei 20 kila mwaka ikiwa ni kumbukumbu ya kusainiwa kwa makubaliano  ya kutumia vipimo vinavyofanana duniani kote ambayo  yalifanywa kutoka mataifa  17 duniani,  tarehe 20 Mei 1875.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad