HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, 23 June 2018

MISS MBEYA 2018 WATUWA TTCL NAKUPIGA JICHO MJENGONI HAPO...

/Volumes/7TOUCHS/Miss mbeya 2018/ttcl/for blog/IMG_1308.JPG
Afisa huduma kwa wateja wa TTCL Corporation Bi Niva Mkwe akiwaelezea
washiriki wa Dream Miss Mbeya 2018 huduma mbalimbali zitolewazo na
shirika hilo.

Meneja wa kanda ya nyanda za juu kusini wa shirika la mawasiliano Tanzania TTCL bwana Juvenal Utafu amewataka washiriki wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania 2018 ngazi ya mkoa wa Mbeya (Dream Miss Mbeya 2018), kuhakikisha wanatumia urembo wao kama nguzo ya kuweza kuzifikia ndoto zao.


Meneja huyo amebainisha hayo baada ya warimbwende hao waliofanikiwa kuingia hatua ya kumi bora ya mashindayo hayo, kutembelea afisi za shirika hilo kanda ya nyanda za juu kusini kwa lengo la kutambua mambo mbalimbali yanayo husu TTCL ikiwa ni pamoja na namna ya uhifadhi wa taarifa za watumiaji wa huduma za mawasiliano.
Bwana Utafu amesema kwamba urimbwende ni moja ya njia za kuweza kuonesha mchango katika jamii, lakini hilo litafanikiwa ikiwa warimbwende hao watajitambua na kusimama vema katika nafasi zao. “Ni lazima mtambue ya kwamba mna deni kubwa kwa taifa, la kutoa mchango chanya katika nyanja mbalimbali, hasa katika hali ya sasa ya dunia ya utandawazi na mapinduzi ya sekta ya mawasiliano”, aliongeza bwana Utafu.
Kwa upande wake meneja msaidizi biashara wa TTCL mkoa wa Mbeya bwana Charles Mwita, alisema kwamba amefarijika sana kwa kauli mbiu wa mashindano hayo isemayo “urembo na kazi kwa maendeleo ya jamii”, na kuwapa changamoto warimbwende hao kwamba hawana budi kuitekeleza kauli mbiu hiyo kwa vitendo.
Juni 29 mwaka huu ni fainali za mashindano ya Dream Miss Mbeya 2018 yenye lengo la kumpata mrimbwende atakayevikwa taji la mrembo wa mkoa wa Mbeya (Miss Mbeya 2018).
Aidha mshindi huyo wa kwanza ataungana washindi namba mbili na namba tatu kuuwakilisha mkoa wa Mbeya katika mashindano ya ngazi ya kanda yanayotarajiwa kufanyika katikati ya mwezi ujao, kuwatafuta wawakilishi wa kanda ya nyanda za juu kusini katika mashindano ya urembo ngazi ya taifa.
Mashindano ya Dream Miss Mbeya 2018 yameandaliwa na redio Dream FM ya jijini Mbeya kwa udhamini wa TTCL Corporation, PII Limited, Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji (TEKU), Ally Rich Sanaa Arts Limited, Kalulu Safari’s Tours Co. Limited, Pepsi, Paradise Inn Hotel, Michuzi Blog, Michuzi Tv, na Dorcus Beauty Point.

/Volumes/7TOUCHS/Miss mbeya 2018/ttcl/for blog/IMG_1545.JPG

Meneja wa kanda ya nyanda za juu kusini wa TTCL C
orporation Bw: Juvenal Utafu akiongea na washirki wa
Dream Miss Mbeya 2018 walipomtembelea ofisini kwake
Jijini Mbeya/Volumes/7TOUCHS/Miss mbeya 2018/ttcl/for blog/IMG_1290.JPG
Meneja msaidizi-biashara wa TTCL Corporation Mkoa wa
Mbeya Bw: Charles Mwita akiwaelezea washiriki wa
Dream Miss Mbeya 2018 huduma mbalimbali zitolewazo
na shirika hilo/Volumes/7TOUCHS/Miss mbeya 2018/ttcl/for blog/IMG_1290.JPG

/Volumes/7TOUCHS/Miss mbeya 2018/ttcl/for blog/IMG_1339.JPG
/Volumes/7TOUCHS/Miss mbeya 2018/ttcl/for blog/IMG_1387.JPG

/Volumes/7TOUCHS/Miss mbeya 2018/ttcl/for blog/IMG_1484.JPG/Volumes/7TOUCHS/Miss mbeya 2018/ttcl/for blog/IMG_1445.JPG/Volumes/7TOUCHS/Miss mbeya 2018/ttcl/for blog/IMG_1539.JPG/Volumes/7TOUCHS/Miss mbeya 2018/ttcl/for blog/IMG_1509.JPG
/Volumes/7TOUCHS/Miss mbeya 2018/ttcl/for blog/IMG_1434.JPG


/Volumes/7TOUCHS/Miss mbeya 2018/ttcl/for blog/IMG_1374.JPG

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad