HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 10 June 2018

PS 3 YABORESHA WATENDAJI WA UMMA NCHINI

Mwezeshaji wa mafunzo ya WISN PLUS POA ,Joram Kiungo toka Tamisemi akitoa somo kwa washiriki wa mkoa wa Dar jinsi ya utoaji wa taarifa za kimfumo katika upangaji wa watumishi katika halmashauri zao Mafunzo ya siku mbili yaliyoanza leo mkoani mtwara na kufanyika katika kanda 6 Nchini na kusimamiwa na tamisemi kupitia mradi wa uboreshaji wa mifumo ps 3 chini ya ufadhili wa USAID. 

Na Abdulaziz Ahmeid, Mtwara
WAKATI Serikali inatarajia kuajiri katika sekta ya afya watumishi wapya 7680 (6180 wa Ofisi ya Tamisemi na 1500 wa Wizara ya afya), halmashauri nchini zimetakiwa kutumia ripoti za mfumo wa WISN plus POA iliyorahisishwa kusambaza watumishi wapya kwa kuzingatia uzito wa kazi na mahitaji kama yalivyoainishwa kwenye taarifa hizo.
Kauli hiyo imetolewa katika kikao kazi kilicholenga kuwasilisha matokeo ya uchambuzi wa mahitaji ya watumishi kwa kutumia mfumo wa WISN plus POA iliyorahisishwa kinachofanyika mkoani hapa.
Mfumo wa WISN plus POA hutumika kukokotoa mahitaji ya watumishi kwa kila kada katika vituo vya kutolea huduma kwa kuzingatia uzito wa kazi katika kituo husika. 
Meneja mradi wa Ps 3 Mkoa wa Lindi Aloyce Mwasuka akifafanua jambo kwa washiriki wa mafunzo hayo ya siku mbili kwa mkoa wa Dar es sallam katika siku ya kwanza ya mafunzo hayo kwa halmashauri zote za mkoa wa Dar es sallam baada ya mkoa wa Lindi kumaliza jana katika ukumbi wa klabu ya bandari manispaa ya mtwara. 

Kwa sasa mfumo huu unatumika kwa ajili ya vituo vya afya na Zahanati tu, ukijumuisha kada mbalimbali zilizopo katika ngazi hizo za utoaji huduma ambazo ni waganga (MO), waganga wasaidizi (AMO), tabibu (CO), tabibu wasaidizi (CA), maafisa wauguzi (NO), maafisa wauguzi wasaidizi (ANO), na wauguzi (EN).
Kikao kazi hicho pia kilitumika kuzijengea uwezo Halmashauri na Mikoa ili ziweze kutumia WISN plus POA iliyorahisishwa kusambaza watumishi wapya, na katika kuomba watumishi wapya.
Akizungumza katika kikao kazi hicho  kilicholenga kuwasilisha matokeo ya zoezi la kubaini mahitaji ya watumishi kwa kutumia mfumo wa WISN PLUS POA iliyorahishwa Mganga Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam  alisema  mfumo huo ni toleo jipya unaowezesha kutumia taarifa kutoka mfumo wa DHIS 2 kwa ajili ya kukokotoa mahitaji ya watumishi, hivyo kupunguza gharama za kutembelea vituo kwa ajili ya kukusanya taarifa.
Mwezeshaji wa mafunzo ya Wisn plus Poa ,Bi Christina Godfrey ,ambae ni afisa program ,sera na uraghibishi PS 3 akitoa elimu juu matumizi ya Tehama ikiwa ni kuwajengea uwezo maafisa utumishi na wataalamu wa afya wa halmashauri za mkoa wa Ruvuma juu ya namna bora ya upangaji wa watumishi katika vituo vya kutolea huduma kwa kuzingatia mahitaji. 

Kikao kazi hicho kilishirikisha  Maafisa Utumishi wa Mikoa na Halmashauri, Waganga wakuu wa wilaya, Makatibu wa Afya wa Mikoa na Wilaya, Waratibu wa MTUHA wa Halmashauri na Wadau wa Maendeleo wa Mradi wa PS3.
Mfumo huo ni sehemu ya Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo katika Sekta ya Umma – “Public Sector System Strengthening – (PS3) unaotekelezwa kwa ufadhili awatu wa Marekani kupitia USAID.
Tayari Halmashauri za mkoa wa lindi,Ruvuma na mtwara zimeshapatiwa mafunzo kwa kanda ya mtwara ikifuatiwa na mikoa ya Tanga na Pwani
Bi Restituta Masao mmoja kati ya wawezeshaji wa mafunzo kwa maafisa utumishi wa mkoa wa Dar es sallam akitoa elimu kwa washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo maafisa utumishi na wataalamu wa afya wa halmashauri za mkoa huo juu ya namna bora ya upangaji wa watumishi katika vituo vya kutolea huduma kwa kuzingatia mahitaji.

Mwezeshaji wa mafunzo ya Wisn plus Poa ,Bi Christina Godfrey ,ambae ni afisa program ,sera na uraghibishi PS 3 akitoa elimu juu matumizi ya Tehama ikiwa ni kuwajengea uwezo maafisa utumishi na wataalamu wa afya wa halmashauri za mkoa wa Ruvuma juu ya namna bora ya upangaji wa watumishi katika vituo vya kutolea huduma kwa kuzingatia mahitaji.

Meneja mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma PS3 mkoa wa Mtwara, Amina Rajabu, pichani akiwa na Bw Peter Henze afisa usafirishaji ps 3 pamoja na Prosper Mbena dereva wa ps 3 wakiratibu baadhi ya masuala ya kiutawala katika mafunzo ya kuwajengea uwezo maafisa utumishi na wataalamu wa afya wa halmashauri za mkoa wa Mtwara juu ya namna bora ya upangaji wa watumishi katika vituo vya kutolea huduma kwa kuzingatia mahitaji katika ukumbi wa benki kuu manispaa ya mtwara chini ya ufadhili wa shirika la Kimarekani la USAID.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad