HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 4 June 2018

MWENGE WA UHURU KUTEMBELEA MIRADI YA THAMANI BILIONI11MKOANI RUVUMA

Na Lituh, Nyasa

Mwenge wa Uhuru umeamenza mbio zake kwenye mkoa wa Ruvuma jana katika kijiji cha Lituhi wilaya ya Nyasa ambapo utatembelea miradi ya maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni11.

Akitoa taarifa ya mkoa kuhusu mbio hizo mkuu wa mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme alisema miradi 20 yenye thamani ya shilingi bilioni 3.2 itazinduliwa,miradi 14 yenye thamani ya shilingi bilioni 4.5 itawekewa mawe ya msingi na miradi 13 yenye thamani ya bilioni 1.5 itafunguliwa na mwenge wa uhuru
Mndeme aliongeza kusema ipo miradi 18 yenye thamani ya bilioni 1.4 itakaguliwa na Mwenge wa Uhuru.
Mkuu wa mkoa huyo alimweleza kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kuwa miradi yote imefanyiwa uhakiki na maandalizi ya kutosha kukidhi ubora unatakiwa.
Alionya watumishi na watendaji wa serekali ambao watabainika kuhujumu miradi ya wananchi au kutumia vibaya fedha za umma kuwa serikali haitosita kuchukua hatua haraka.
"Katika utekelezaji na usimamizi wa miradi ya maendeleo ya wananchi kwenye mkoa wangu sitomvumilia mtumishi atakayeharibu miradi na kufuja fedha" alisisitiza Mndeme
Mkuu wa mkoa alieleza pia kuwa mkoa unaendelea na kazi ya kauli mbiu ya mwaka huu kusimamia elimu kwa kuhakikisha sera ya elimu bila malipo inatekelezwa kote kwa watoto kupelekwa shule bila vikwazo.
Kuhusu mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI mkoa wa Ruvuma una maambukizi ya asilimia 5.5 kiwango ambacho ni kikubwa zaidi ya kile cha kitaifa asilimia 4.7 ambapo mikakati ya kudhibiti inatekelezwa pamoja na wadau.
Kwa upande wake kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Chares Kabeho ameupongeza mkoa wa Ruvuma kwa kuwa miongoni mwa mikoa yenye utoro hafifu wa wanafunzi mashuleni.
Ameagiza mkoa kuhakikisha unasimamia mkakati wa upatikanaji wa chakula mashulen kama ilivyofanikiwa mikoa ya Njombe na Kilimanjaro.
"Ruvuma mnacho chakula cha kutosha lakini shule zenu nyingi hazitoi chakula kwa wanafunzi,igeni kwa Njombe na Kilimanjaro namna walivyofanikiwa" alisema Kabeho
Kabeho alisema Serikali ya awamu ya tano ya Rais John Pombe Magufuli inataka wazazi na walezi kuchangia chakula kwa ajili ya watoto wao na hii itasaidia kukuza taaluma na kuondoka mdondoko wa watoto kutimiza ndoto zao.
Mwenge wa Uhur utakimbizwa umbali wa kilometa 1,27 katika hlmashaur nane za mkoa wa Ruvuma.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad