HABARI MPYA

Home Top Ad



Post Top Ad

Thursday, 14 June 2018

Mjumbe wa Katibu Mkuu UN ahimiza ushirikiano kukabili uhalifu

Na Mwandishi wetu
MJUMBE maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa nchi za Maziwa Makuu (ICGLR), Said Djinnit ametaka nchi wanachama wa Umoja wa Ushirikiano katika masuala ya kisheria katika nchi hizo za ICGLR , kuongeza kasi ya mashirikiano ili kukabiliana na uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Nchi zinazounda umoja wa ICGRL pamoja mwenyeji Tanzania ni Angola, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya kati, Congo, Kenya, Rwanda, Sudan, South Sudan, Uganda na Zambia.
Alisema pamoja na kufikia maendeleo ya kutosha katika ushirikiano wa kisheria nchi hizo kwa sasa zinatakiwa kuungana zaidi kutokana na watenda uhalifu dhidi ya ubinadamu kuendelea kujificha katika nchi mbalimbali.
Akizungumza katika mkutano wa pili wa umoja huo uliofanyika jijini Dar es salaam jana, Djinnit alisema kwamba mambo makubwa mazuri yamefanyika miongoni mwa nchi hizo tangu kuuanzishwa kwa ushirikiano huo, na kutaka wazidi kujiimarishwa sanjari na ushirikiano mwingine wa kukomesha uhalifu.
Alisema bila kukomeshwa kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu mataifa ya Maziwa makuu yatakuwa katika hekaheka na hiyvo kukosa maendeleo kutokana na kukosekana kwa amani.
Awali akmimkaribisha mjumbe huyo kufungua mkutano, Naibu Mkurugenzi Mwendesha Mashtaka nchini Tanzania, Frederick Kapela Manyanda alishukuru ushiriki wa wajumbe wa wataalamu wa sheria kutoka nchi za ICGLR akisema ujio wao ni neema ya kufanikisha ushirikiano dhidi ya vitendo vya kihalifu.
Akishukuru ujio wa mataifa hayo katika nchi ambayo imekuwa ikijishughulisha sana na upatanishi kwa majirani, alisema mkutano huo una maana kubwa kwa kuwa utaongeza msukumo katika kukabiliana na uhalifu wa kimataifa.
Alisema ingawa huo ni mkutano wa pili katika kuunganisha juhudi za kukabiliana na uhalifu alisema umoja huo una maana zaidi kwa kuangalia wengine duniani wamefanya nini, na kutolea mfano wa kuwapo wa West African Network of Central Authorities and Prosecutors (WACAP) unaofanyakazi sanjari na mamlaka ya ECOWAS.
Alisema kutokana na ukubwa wa nchi na mipaka mataifa ya Great lakes ni lazima kushirikiana ili kuhakikisha kwamba hakuna mtu au kitu kinajificha katika maeneo yao chenye lengo la kuharibu usalama wa mataifa hayo.
Alisema  zipo rabsha na zinatishia amani na kusema mpaka hapo vitendo hivyo vitakapodhibitiwa kwa pamoja ndipo maendeleo ya kweli yatapatikana.
Alitaka wajumbe kuangalia namna ya kushirikiana katika nyanja zote na kwa kutumia weledi na utaalamu  ili kudhibiti vitendo vya kihalifu dhidi ya binadamu.

Ukiwa ni mkutano wa pili kufuatia uliofanyika Khartoum Sudan Novemba 2017, wajumbe wanatarajia kuangalia itifaki mbalimbali na kuzipa nguvu ili ziweze kusaidia katika kukabiliana na viashiria vya uvunjifu wa amani
 Naibu Mkurugenzi Mwendesha Mashtaka nchini Tanzania, Frederick Manyanda akitoa neno la ufunguzi wakati wa mkutano wa pili wa ushirikiano wa kisheria nchi za maziwa makuu (ICGLR) unaoendelea katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam
 Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa ICGLR, Bi. Eliane Mokodopo akizungumza kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa ICGLR, Balozi Zachary Muburi-Muita (hayupo pichani) wakati wa mkutano wa pili wa ushirikiano wa kisheria nchi za maziwa makuu (ICGLR) unaoendelea katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Mjumbe maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa nchi za Maziwa Makuu (ICGLR), Said Djinnit akizungumza wakati wa mkutano wa pili wa ushirikiano wa kisheria nchi za maziwa makuu (ICGLR) unaoendelea katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Uholanzi nchini, Mh. Jeroen Verheul akitoa salamu za taifa la Uholanzi wakati wa mkutano wa pili wa ushirikiano wa kisheria nchi za maziwa makuu (ICGLR) unaoendelea katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja (UNDP), Alvaro Rodriguez akibadilishana mawazo na mmoja wa wajumbe wa mkutano wa pili wa ushirikiano wa kisheria nchi za maziwa makuu (ICGLR) unaoendelea katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Kutoka kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mwendesha Mashtaka nchini Tanzania, Frederick Manyanda, Mwakilishi wa Katibu Mtendaji wa ICGLR, Bi. Eliane Mokodopo pamoja na Balozi wa Uholanzi nchini, Mh. Jeroen Verheu wakati mkutano wa pili wa ushirikiano wa kisheria nchi za maziwa makuu (ICGLR) unaoendelea katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP), Natalie Boucly (kulia) na wajumbe wengine wakifuatilia kwa umakini hotuba mbalimbali zilizokuwa zikiwasishwa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa pili wa ushirikiano wa kisheria nchi za maziwa makuu (ICGLR) unaoendelea katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Balozi wa Marekani nchini Immi Patterson (kushoto) akiandika mambo muhimu wakati wa mkutano wa pili wa ushirikiano wa kisheria nchi za maziwa makuu (ICGLR) unaoendelea katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja (UNDP), Alvaro Rodriguez akipitia makabrasha wakati wa mkutano wa pili wa ushirikiano wa kisheria nchi za maziwa makuu (ICGLR) unaoendelea katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.


 Pichani juu na chini ni sehemu ya washiriki kutoka nchi zinazounda umoja wa ICGRL pamoja mwenyeji Tanzania, Angola, Burundi, Jamhuri ya Afrika ya kati, Congo, Kenya, Rwanda, Sudan, South Sudan, Uganda na Zambia wakati wa mkutano wa pili wa ushirikiano wa kisheria nchi za maziwa makuu (ICGLR) unaoendelea katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja (UNDP), Alvaro Rodriguez (kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP), Natalie Boucly wakati wa mkutano wa pili wa ushirikiano wa kisheria nchi za maziwa makuu (ICGLR) unaoendelea katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad