HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 12, 2018

Mawakala Halo pesa sasa kuweka na kutoa fedha kupitia NMB

Katika kutekeleza azma ya  kuboresha utoaji huduma za kifedha kwa wananchi wenye vipato tofauti,  Kampuni ya mawasiliano ya Halotel na benki ya NMB zimeingia katika ushirikiano  utakao wawezesha mawakala wa Halo Pesa kutumia huduma za kibenki za NMB kupitia "huduma kabambe kwa Wakala" (Super-Agency service.) kwa ajili ya kuweka na kutoa fedha kupitia benki hiyo.

Hatua hii itawawezesha mawakala wote wa huduma za kifedha kupitia Halo Pesa  nchi nzima kuweza kuweka na kutoa pesa taslim kupitia tawi lolote la benki ya NMB na kuweza kuwanufaisha mamilioni ya watanzania na huduma za kifedha  kwa njia ya mtandao kwa ukaribu na urahisi zaidi.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Halo Pesa, Vu Tuan Long, amesema Ushirikiano huo ni hatua nyingine kubwa katika utoaji wa huduma za kifedha kupitia mawakala  ambapo sasa  huduma ya  kutoa na kuweka pesa kwa mawakala zitafanyika kupitia benki ya NMB.

"Huduma za   kifedha  kwa njia ya mtandao ni  sekta  inayokua  kwa  kasi hapa  nchini. Ushirikiano huu utawawezesha Mawakala wa Halo Pesa kuweza kupata huduma ya kuweka na kutoa pesa kiurahisi kupitia matawi yote ya NMB nchi nzima “Alisema Long.

Mpaka hivi sasa Halotel ina mawakala zaidi ya 55,000 walioenea nchi nzima. Mawakala wa HaloPesa watatumia namba za USSD za Halo Pesa ambazo ni (*150*88#) kwa kutoa fedha katika benki ya NMB pamoja na kutoa fedha, kwa fomu maalumu za kuweka fedha wakiwa katika matawi ya benki ya hiyo.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa wateja wa kati na wadogo wa benki ya NMB Boma Raballa, amesema benki ya hiyo imekuwa ya kwanza katika kutoa huduma zenye ubunifu ambazo zinalenga kutatua changamoto mbalimbali ndani ya jamii, Tulitambua kuna uhitaji katika upatikanaji wa fedha kwa mawakala” Alisema Raballa.

“Mtandao mkubwa wa matawi yetu unaoenda sambamba na kauli mbiu yetu ya “Karibu Nawe” imekuwa sehemu kubwa ya mafanikio katika utoaji wa huduma za kifedha. Hadi sasa tuna matawi Zaidi ya 220 ambayo yako kwa Zaidi ya asilimia 98 ya wilaya za nchi hii zitarahisisha sana upatikanaji wa huduma kwa mawakala”. Alisema Raballa.

Nchi ya Tanzania ni miuongoni mwa nchi zinazoripotiwa kuwa na watumiaji wengi wa huduma za kifedha wakifikia Takribani milioni 19, hivyo uhitaji na upatikanaji wa fedha kwa watumiaji hao imekuwa ni changamoto kubwa kwa baadhi ya watumiaji, Kupitia benki ya NMB sasa mawakala na watoa huduma za kifedha sasa watakuwa na nafasi ya kupata huduma karibu yao.
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Halotel Mhina Semwenda akitoa ufafanuzi  mbele ya mkutano wa waandishI wa Habari katika  uzinduzi wa kusaini  mapatano ya ushirikiano baina ya Halotel (Halopesa) na benki ya NMB, utakao wawezesha mawakala wa Halopesa nchi nzima kutumia huduma za kibenki (kutoa na kuweka pesa) kupitia tawi lolote la benki ya NMB . Kushoto  ni Kaimu mkuu wa wateja wa kati na wadogo  kutoka benk ya NMB.
aibu Mkurugenzi wa Kitengo cha huduma za kifedha Vu Tuan Long(kulia) na Kaimu Mkuu wa wateja wa kati na wadogo wa benki ya NMB wakibadilishana mkataba wa makubaliano ya ushirikiano katika  uzinduzi wa kusaini  mapatano ya ushirikiano baina ya  Halotel (HALOPESA) na benki ya NMB. Ambapo mawakala wa Halopesa wataweza kupata huduma za kifedha kupitia tawi lolote la NMB nchini. (Kulia) Meneja wa Kitengo cha Mawasiliano Mhina Semwenda, (kushoto) moja ya mwakilishi kutoka Benki ya NMB

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad